Hapo itabidi tuanza kuzungumzia Qadar...., Utayari...Kujitoa....Malengo...Ufanisi....Namna ya kupokea changamoto za biashara za kuzitatua..n.k
Pia tutatakiwa kujikita kwenye ukweli kwamba si Kila mtu amezaliwa kuwa mfanyabiashara...
Kuna wale wanazaliwa biashara ipo kwenye damu huyu ni ngumu sana kukata tamaa na kutofanikiwa kwenye biashara.
Kuna wale wanatamani kufanya biashara na wanajaribu kufanya biashara ila hawawezi biashara Hawa ndio unakuta baada ya muda mfupi biashara Hana, au Leo anafanya hiki, kabla hakijasimama anaacha anahamia kule, kule nako hakujakaa vizuri anahamia biashara nyingine.
Biashara haihitaji pesa tu, inahitaji moyo wa dhati Kwa kuwa Kuna kukatishwa tamaa mno, Kuna changamoto nyingi sana Hadi kuanza kuona matunda ya biashara, ni biashara chache ambazo zitanyooka tu tangu mwanzo.
Nadhani nimejaribu kukujibu mkuu, kadri ya ufahamu wangu.