SoC02 Kufanikiwa pasina kutimiza wajibu kwa kiwango kinacho stahili

SoC02 Kufanikiwa pasina kutimiza wajibu kwa kiwango kinacho stahili

Stories of Change - 2022 Competition

Franknel

New Member
Joined
Aug 22, 2022
Posts
1
Reaction score
1
MAFANIKIO Nikuweza kuyafanya malengo(Maono), mikakati au mawazo kuwa halisi katika Maisha, lakini WAJIBU Ni jumla ya majukumu yanayo mpasa mtukuyatimiza baada ya kupokea haki fulani Mfano Katika familia mtoto anayo haki yakupokea mahitaji kutoka kwa wazazi naye anao wajibu wa kuwasikiliza na kuwaheshimu.

Katika maisha kila kiumbe huwa na nia au malengo ambayo huyapanga yaweza kuwa ya muda mrefu au mfupi, malengo hayo hutazamia kuyatimiza kwa muda husika na katika jinsi(namna) anayo itaka kutokana na mtazamo wake, mtazamo hupelekea watu wawili au zaidi kuwa na aina moja ya lengo lakini kila mmoja akawa na namna yake yakutekeleza, kwa mfano wanafunzi wa wawili wenye lengo la kufahulu, mwanafunzi wa kwanza anaamini ili afahulu a nahitaji masomo ya ziada(tuition) na wa pili anaamini katika masomo ya darasani na mazoezi ya mara kwa mara ukiangali njia zote mbili ni sahihi na kila mmoja akifuatilia kwa usahihi atafanikiwa kufahulu.

Kuwa na malengo katika maisha ni kawaida ya kila mtu au kiumbe chochote, kuwa na malengo humleta mtu katika uwezekano wa matokeo mawili ambayo ni KUFANIKIWA au kushindwa kufanikiwa(kufeli) au pia muda mwingine huwa ni kufahulu chini ya kiwango au kipimo alichokiweka mtu husika hii naweza nikasema ipo katikati ya kufanikiwa na kufeli tukirejea mfano wa wanafunzi walio lenga kufahulu kama mmoja wa wanafunzi alipanga kufahulu kwa wastani wa "A" ila akapata wastani wa "C" mwanafunzi atakuwa amefanikiwa kufahulu ila kafeli kutimiza kiwango cha lengo lake
Kushindwa kufika malengo(kufeli) huwa ni matokeo mzito kuyapokea na pia huleta huzuni.

Hapa mtu huweza kukatatamaa au akarudi nyuma na kutafuta alipokosea ili kurekebisha kama bado kuna nafasi ya kufanya hivyo, kufeli kutimiza malengo ni kitu kimoja wapo kinachosumbua katika mzunguko wa maisha, hii hutokana na asili ya viumbe vyote hususani Binadamu.Vitu hivi vifuatavyo ni bahazi ya vitu muhimu ambavyo kila kiumbe huitaji katika MAISHA ambayo ndiyo asili vitu hivi ni.

ULINZI Kila kiumbe hupenda kijihakikishia ulinzi katika maisha yake, ulinzi unaweza kuwa kimawazo kimwili na kadhalika hutofautiani kutokana na umri, jinsia na mtazamo, mtu au kumbe chochote kinapo shindwa kijihakikishia ulinzi huwa ni ishara mojawapo ya kufeli.

UTOFAUTI Binadamu anahitaji utofauti katika maisha, utofauti huwa kimtazamo, mwonekano, ulaji,na kadhalika mtu anaposhindwa kuwa tofauti katika hali mbali mbali zinazo mahitaji kuwa tofauti hii pia huwa alama ya kufeli.

UMUHIMU, HESHIMA na UTAMBULIKAJI Kila kumbe kina UMUHIMU wake katika mzunguko wa maisha, kwa hivyo kila kumbe huitaji kuheshimika na kutambulika kutokana na umuhimu wake katika mazingira yake, bali kufeli humfanya Binadamu kuhisi kupunguza umuhimu wake katika mazingira yake, hii hupelekea kijihisi kukosa hashima na utambulikaji katika maisha.

UPENDO na KUKUBALIKA Huu ni uhalisia wa kila kiumbe hususani Binadamu, kila mtu hutegemea upendo na kukubalika zaidi sana kwa watu wake wakaribu mtu anapofeli hukosa kukubalika na pia upendo hupungua kwa bahadhi ya watu.

KUKUA na KUONGEZEKA Ni maneno mawili yanayo enda sambamba na kuleta mjumuisho wa maana ya kufanikiwa, naweza nikasema Kukua ni kutoka hatua moja kwenda nyingine lakini Kuongezeka ni kuendelea kustawi katika hatua iliyo ifikia. Kwa mfano mtoto mwenye umri wa miaka mitano na uzito wa kilogram 11 inawezekana akiwa na miezi mitatu kabla hajafika miaka sita akuwa na uzito wa kilogram 13 mtoto atakuwa ameongezeka ila hajakua hivyo basi kushindwa kukua na kuongezeka ni mojawapo ya ishara ya kifeli.

UWEZO na UCHANGIAJI Kila mtu hutaka kuwa na uwezo wa kufanya vitu mbali mbali ambayo vipo ndani ya uwezo wake ambavyo baadae hupelekea uchangiaji katika mazingira yake kwa hivyo mtu akifeli kwa namna fulani humfanya kushindwa kuchangia katika mzunguko wake wa maisha.

Baada kuona jinsi gani kufeli kunaathiri mzunguko wa maisha sasa tuone kitu kingine kinacho athiri mzunguko wa maisha baada ya mtu kushinda tatizo la kufeli ambacho ni KUSHINDWA KUWAJIBIKA KATIKA KIWANGO KINACHO STAHILI BAADA YA KUFANIKIWA, jaribu kutafakari vitu hivi. Je kwa nini?
  • Kiongozi anayependwa na kukubalika na watu wake bado hutafuta jinsi ya kuwa mwadilifu katika nyanja mbali mbali kwa watu wake
  • Mfanyabiashara aliyefanikiwa kwa kiasi kikubwa kidunia bado hutafuta mifumo na mikakati ya kuzidi kuboresha na kuongezeka
  • Mwanafunzi aliyefanikiwa katika elimu yake na kuwa bora mfanisi na enayekubalika katika tasnia yake (ufundi, afya na uchumi) bado huzidi kusoma na kutafuta kukua zaidi katika tasnia yake
- Mwanamichezo anayeaminika kuwa ni kinara katika uchezaji wake bado hutafuta kujiongezea ujuzi na mazoezi zaidi. Mwaswali hayo yote yanaweza yakawa na majibu mbali mbali kutokana na mtazamo wa kila mtu, kwa mfano kwa Mfanyabiashara na Mwanamichezo bora unaweza kusema ni kwasababu ya ushindani na kwa Kiongozi bora unaweza kusema labda azidi kujihakikishia nafasi yake katika jamii au watu wake, ila kwa mwanafunzi bora, mfanisi na anayekubalika na kuaminika katika tasnia yake yeye hufanya hivyo kwa ipo ndani ya uwezo wake na matamanio yake ni kufanya hivyo katika kiwango chake cha juu kutokana na uwezo wake aliokuanao ili uchangiaji wake katika mazingira yake uwe ubora na katika kiwango kinacho stahili kutokana uwezo wake(maarifa, ujuzi mbinu n.k)

Ndugu na jamaa katika maisha ya watu mbali mbali walio fanikiwa katika nyanja tofauti, ukiachana na sababu nyingi zinazo wafanya kutaka kukua zaidi sababu hii ya KUWAJIBIKA katika kiwango cha juu kutokana na uwezo wao ndio huwaskuma zaidi kutokana na imani yao katika uwezo wao hivyo huzidi kujituma na kuongeza bidii katika kukabiliana na vikwazo na changamoto mbali mbali hakikisha utumiaji bora wa rasirimali zao kama muda, ujuzi na zingine mbali mbali.

Tuchukulie mfano Mdogo Wazazi kaitaka familia nyingi za kiafrika na Dunia kwa ujumla Baba huwajibika katika kuhakisha ustawi wa familia na kuhakikisha familia inaishi katika hali bora na yakuruzisha ndo maana Kila siku huzidi kuongeza bidii katika kuwekeza katika rasirimali tofauti tofauti ili uchangiaji wake katika ustawi wa familia uwe wa uakika.

Ndugu na jamaa baada ya kuona kuwa uwajibikaji katika kiwango cha juu katika mambo yale ambayo tumefanikiwa ni mzizi Mkubwa katika ustawi wa maisha ya mtu binafsi, Taifa na Dunia kwa ujumla, kwa hiyo ndugu na jamaa tuzidi kujituma na kuwajibika zaidi katika yale ambayo tumefanikiwa ili uchangiaji wetu katika maisha yetu binafsi,Taifa na Dunia uwe Mkubwa na wenyemanufaa.

Ili mtu kuweza kuwajibika katika kiwango chake cha juu inabidi ahakikishe a natumia rasirimali zake hususani Muda kikamilifu. JE, KWA UWEZO NA MAFANIKIO ALIYOKUJALIA MUNGU UMEWAJIBIKA KATIKA KIWANGO CHAKO CHA JUU. Kila mtu akiwajibika katika yale aliyo fanikiwa ubunifu utazidi zaidi, ufanisi utazidi na kwa hivyo jamii, Taifa na Dunia kutakuwa na Mafinikio zaidi.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom