Kufanikiwa sekta ya burudani ni ngumu.

Trayvess Daniel

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
651
Reaction score
1,244
Kwenu wanajamvi... ni mtazamo tu.

Walengwa wakubwa hapa ni wanamuziki na wanafilamu.

Nikianza na wanafilamu, hawa sanaa yao imepoteza mvuto siku nyingi kinachofanyika ni kurudisha mvuto.

Hata pale mtu anapojitahidi kurudi mashabiki wamekua wepesi kukosoa mambo ambayo hayahusiani na filamu. Mfano jana wema kazindua movie lakini nguvu kubwa imeelekezwa kukosoa na kusifia mavazi lakini team yake haijaungana kupromote kazi yake.

Chuki binafsi pia zimetawala, mf shabiki asipompenda msanii fulani hata atoe kazi nzuri hatosupport kamwe.

Maisha binafsi kuzidi kazi. Page zimekua za maisha binafsi kupitiliza kiasi kwamba shabiki unajua idadi ya wanaume ya msanii kuliko movie zake.

Anapoteza mvuto katika jamii hata movie ikitolewa inapuuzwa.

Mwisho hawa wasanii huwa hawatoi mrejesho ya filamu zao. Ukiwaambia mashabiki wako umeuza kiasi gani na changamoto zipi zilizopo inasaidia ukitoa kazi mpya.

WANAMUZIKI
hapa ni changamoto, adui namba moja ni team kiba team mondi. Huu uteam unaua wasanii wengine kuonekana ambao huwa wanatoa ngoma nzuri kuliko wahusika nyakati fulani.

Diamond wewe tunajua unajua anataka nini na njaa yako ni ya kudumu na utafika mbali acha mipasho na chokochoko na timu pinzani sababu mwisho wa siku wao ndo wanafaidika. Achieni nafasi na wengine wang'are.

Bongo hakuna kitu inaitwa bifu ya kibiashara mashabiki always take things personal.

Chuki binafsi kwa waliofanikiwa. Wasanii waliofanikiwa hawapendwi na wengi na hili huwa linadhihirika wanapokosea, nguvu kubwa hutumika kukosoa kuliko kujenga. Ifike hatua kizuri na kibaya viwe vinaainishwa sio vibaya tu.

Mf ngoma ya Vanessa ya kisela ilipondwa sana lakini ukiangalia bado ina mengi mazuri achilia mbali mapungufu.

Kiki zisizo na msingi. Mziki mzuri unajiuza sio kila mara kutegemea kiki ili kutoa wimbo, hii ni kiashiria cha udhaifu. Promote wimbo inavyopaswa na sio kwa kiki za kipuuzi.

Maisha binafsi kuzidi muziki. Hii ni kama bongo movie, msanii unamfahamu kwa maisha binafsi kuliko kazi zake.

Mwisho mashabiki wa bongo ni wachache na kipato pia ni changamoto, hao mashabiki ni ngumu kujigawa kushabikia movie, mziki, maisha binafsi ya msanii, ugomvi n.k na kati ya hao mashabiki wachache bado mashabiki maandazi ambao kazi yao ni maneno tu na hawasupport kazi za wenzao mfano mzuri mashabiki wa wema.
 
Diamond na kiba nyimbo wanazotoa ni za kawaida tu, ila beef linawabeba, kinachoniuma zaidi media na watangazaji nao wameingia ktk mkumbo huu na baadhi ya wasanii wengine wapumbavu nao wana chagua pande. Inatakiwa hawa waachwe wenyewe wawili wapambane wenyewe na hali zao kwani likiendekezwa beef litaua mziki wetu, kwani wasanii wengine hata watoe nyimbo kali namna gani hazitosikika, ww nyimbo kama ya Jux bonge la nyimbo lkn media na watangazaji wamelikaushia. Hata mwaka jana nyimbo kama samaki ya galatone, lover boy barnaba, sisikii maua sama na nyinginezo nyingi hazikupewa airtime za kutosha kutokana na media na watangazaji kuwa ktk timu hizi . yaani tunapoelekea tukiendelea na ushabiki huu mziki utakuwa wa kiba na mondi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…