Kufanya haya mwanaume haipendezi. . . (Mwendelezo wa sisi ni wanaume bwana!)

Kufanya haya mwanaume haipendezi. . . (Mwendelezo wa sisi ni wanaume bwana!)

Calnde

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2008
Posts
1,373
Reaction score
278
Kuna uzi uliokuwa unasema sisi ndo wanaume bana! Mimi naomba niendeleze kwa kutoa yale nnayodhani hayafai kwa mwanaume kufanya. . .
1. Haipendezi kubana matumizi kwa familia lakini kutumia kwa issue nyingne kama kupiga maji, gari nk

2. Haipendezi mwanaume kutokuwa na utaratibu wa kuwa na refreshment na familia yako

3. Haipendezi mwanaume kuvaa vijinguo vya kubana kama 'skinitait' eti fashion

4. Haipendezi mwanaume kuwakusanya wenzio na kuwahadithia unavyo 'm-do' mkeo au mpenzi wako.

5. Na hii tabia ya wanaume kujipodoa kupitiliza, sijui kujichubua, lipshine, kuweka dawa nywele za kiafrika, kuvaa hereni pia naona haipendezi.

6. Wanaume mnatembea barabarani mnashikana shikana mikono, mara kukumbatiana (kumbuka hapa simaanishi kwa kusalimiana) haipendezi.

7. Mwanaume kuwa mmbea, haifai

8. Kupiga mkeo, aah mbaya sana

Waweza endeleza
 
kuwa na wivu kupita kiasi kwa mwenza wako bila sababu za msingi... mpe space!
 
9. Haipendezi mwanaume kuwa na lugha chafu isiyokuwa na staa

10. Haipendezi mwanaume kurudi usiku wa manane kila siku kiasi kwamba watoto wanakusahau

11. Haipendezi mwanaume kukana mimba wakati umegonga kavu...
 
haipendezi mwanamme kutaka/kumruhusu mkewe ajichubue wakati alimwoa mweusi.
 
haipenezi mwanamme kuruhusu watoto wake under 14 kujiingiza kwenye urembo ulopitiliza kiasi kwamba wakiwa wakubwa ndio wanakuwa akina maiko jakisoni.
 
Haipenezi mwanamme kutongoza kila mwanamke anayepita mbele ya uso wake.
Kana kwamba hajui simba mzee ndo hula nyama.
 
haipendezi mwanamme kukopa pombe, au spea ya gari au dada poa.
 
haipendezi mwanamme kufika miaka 45 bado hajajenga hata kama ni kibanda cha tope, hii huonyesha kiwango chake cha malengo na yuko 'realistic' kwa kiwango gani.
 
haipendwzi.mabisa mwanaume kuoa mke mwenye roho mbaya
 
hapendezi kabisa mwanaume kuwa demu asiyejua kujisafi
 
Back
Top Bottom