MOTTO: Kijana na mabadiliko ya uchumi.
LENGO: Kusaidia kukua kiuchumi vijana walio hitimu kidato cha nne na kufeli mitihani yao wakiwemo pia vijana wa makundi maalum na wapo nyumbani hawana vyanzo vya kujiingizia vipato na kuwabadilisha kiuchumi wale wasio na elimu kabisa.
DIRA: Kuhakikisha mabadiliko ya kiuchumi yanafanyika nchini kwa kuanza na vijana waliopata angalau elimu ya kidato cha nne wakiwemo pia wa makundi maalumu bila kujali jinsi na baadae wao kuwabadilisha kiuchumi pia wale ambao hawakupata elimu kabisa kwa kufanya nao kazi mbalimbali za kujipatia kipato na elimu ya kujitegemea.
Mimi naitwa Cosmas Flavian Komba, ni kijana wakiume, mtanzania na nina umri wa miaka 38. Elimu yangu ni stashahada ya elimu ya sekondari na ninaishi Galapo Babati Manyara.
Kama nilivyo onesha kwenye kichwa cha habari baada ya kuona vijana wengi wanapita na kuteseka na maisha, nipo tayari kujitolea kuibadilisha jamii kiuchumi kupitia ajira na elimu ya kujitegemea.
Nitaanza na vijana wanao nizunguka waliomaliza kidato cha nne na kutopata matokeo mazuri ambayo yaliwafanya wao kukosa sifa za kuendelea mbele kimasomo.
Nikiipata hiyo hela ya kiasi cha shilingi 5,000,000/= itakuwa kama mtaji ambao ntautumia kuwabadilisha vijana hao kiuchumi na waweze kujitegemea.
Ningependa weka wazi kitu ambacho ntafanya nao na kuwabadilisha na wao kuwabadilisha vijana wengine ambao hawakuweza pata elimu au walikatisha masomo yao kwasababu nyingi kama mimba za utotoni, madawa ya kulevya na umasikini.
Nitanunua Mashine ya kutotolesha vifaranga na nitaiweka kwenye eneo ambalo lipo tayari na linaumeme kabisa, kupitia mashine hiyo nitaanza na vijana 20 katika mradi huu, mradi unavyozidi kukua nitaongeza vijana wengine na hata wale ambao hawana elimu kabisa nitawapa elimu ya vitendo na kujitambua umuhimu wake kama vijana.
Ufuatao ni mchanganuo wa shilingi 5,000,000/= itakavyo tumika,
1,000,000 - Kununulia mashine ya kutotolesh vifaranga ya mayai 352 na usafiri wa kuileta Galapo babati Manyara.
2,200,000 - Kujengea Banda bora la mfano la kufugia hao kuku.
100,000 - Vifaa vya kulishia na kunyweshea.
100,000 - Tiba kwa vifaranga.
1,000,000 - Mavazi maalumu, buti na vifaa vingine vya kuvaa na dawa ili kujifunza vyema na kuepusha vimelea vya magonjwa kuwafikia kuku.
550,000 - Chakula cha kuku kuanzia wadogo hadi kufikia kuuzwa.
50,000 - Umeme.
Huu mchanganua ni mwanzo wa kuanza mradi wetu, baada ya kukua hao kuku mradi utajiendedha vyema kabisa wenyewe kwa kuuza mayai, vifaranga na kuku wakubwa, kutotolesha mayai kwa wafugaji wengine, kuuza mbolea itokanayo na kinyesi cha kuku, kuanzisha bustani za mbogamboga tutaongeza aina mbalimbali za mifugo kama kanga, sungura,kondoo,mbuzi na ng'ombe.
Pia tutakisajili na kutoa vyeti na kuhakikidha kutoa japo mashine chache za kutotolesha vifaranga kwa wahitimu kila mwaka ili wajiunge kimakundi na kujiajiri. Pia na kupokea wahitimu wapya na tutakuwa tunaongeza mashine za kutotolesha kuendana na ukubwa wa soko.
Mwisho napenda kushukuru kwa jambo hili mlilolitoa kwani kwenye jamii tunazoishi na zinazotuzunguka kuna ndoto nyingi zenye malengo chanya kabisa kwa vijana na hata watu wengine kama wazee na makundi maalumu, ila tatizo huwa ni mtaji.
Naimani mtalisoma andika langu, mtalifanyia kazi na linaweza shinda kabisa ili tusaidie vijana hawa kwani wanahitaji sana elimu ya kujitegemea katika safari yao ya kujikomboa katika umasikini, na kuelekea kwenye uchumi mzuri na kuwa na familia bora ambazo zitaleta vizazi bora kwa manufaa ya Taifa zima.
Asanteni sana, na naimani andiko langu litapitiwa vyema na kufanyiwa kazi.
Simu: 0689772886

Upvote
0