Kufanya Overhaul: Je ni sahihi kwa muktadha huu!!?

Kufanya Overhaul: Je ni sahihi kwa muktadha huu!!?

worms

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2017
Posts
978
Reaction score
911
Habari wakuu.

Natumia gari aina ya Rav 4 kilitime engine 1790cc vvti.
Baada ya kuiendesha muda mrefu kidogo maji yalikuwa yanavuja na hivyo ilichemka sana bila mimi kujua.

Nimepeleka kwa fundi ananiambia natakiwa kufanya engine overhaul, Je ni sahihi? Na gari kuchemka muda mrefu inapelekea uhitaji wa kufanya overhaul?
 
Mbona mwapita hivi hivi
 
Either hiyo gari imeunguza gasket hivyo kufanya oil kuchanganyika na maji.......

Ikiwa hivi mzee hamna namna nyingine zaidi ya kuimwaga chini ENGINE
 
Pole sana...

Kama gari ilichemka... hapo vya kucheki ni:
- Cylinder head kama ilipata cracks...

- Unaifanyia overhaul gasket... ambayo inakaa between the engine block na cylinder head...

Kama engine ili knock out... ndiyo mambo ya piston, sleeves, rings na cylinder vinahusika...

Cc: mahondaw
 
Either hiyo gari imeunguza gasket hivyo kufanya oil kuchanganyika na maji.......

Ikiwa hivi mzee hamna namna nyingine zaidi ya kuimwaga chini ENGINE
Nimeambiwa na fundi kuwa ilikuwa inachanganya maji na oil pia
 
Pole sana...

Kama gari ilichemka... hapo vya kucheki ni:
- Cylinder head kama ilipata cracks...

- Unaifanyia overhaul gasket... ambayo inakaa between the engine block na cylinder head...

Kama engine ili knock out... ndiyo mambo ya piston, sleeves, rings na cylinder vinahusika...

Cc: mahondaw
Nashukuru ndugu
 
Paki gari tafuta pesa nunu engine mpya, replace urudi barabarani. Ukianza sijui overhaul utakuwa kila uchao unakuja hapo gereji.
Sahihi kabisaaaaa... Yangu ilianza kusmoke, fundi akaniambia nifanye overhaul tuweke rings nyingine..

Injini ipo stoo nimeweka used from japan na maisha ni kama nimetoka bandari tena.
 
Sahihi kabisaaaaa... Yangu ilianza kusmoke, fundi akaniambia nifanye overhaul tuweke rings nyingine..

Injini ipo stoo nimeweka used from japan na maisha ni kama nimetoka bandari tena.
inategemea na uwezo wa fundi kama fundi anafaham anachokifanya engine inafanyiwa overhaul na inarudi sawa bila shida sema unakuta gareji bubu mtu hana hata engine pressure test alafua anakuambia anafanya overhaul, nimesha badili block nyingi za 2az na gari zipo barabarani hadi Leo maana hizi engine model za mwanzo bolt zilikuwa zinafunga thread chache hivyo kupelekea cylinder head kuvuta bolt za upande mmoja na gari huanza kuvuja maji au oil, wengi wamekuwa wakipeleka kuweka bush ila mm nimekuwa nikiwashauri bora ununue block then hamishia vitu kwenye new block, sasa unakuta MTU kagari kana engine yenye 990cc alafu imetembea 200,00+ alafu unajiganga hii engine haijawahi funguliwa hivi mnazani kitu kama piston ring hazichoki? Au anakuja kuanzisha mada " ka passo kanakura mafuta balls"
 
Kama gari inachemka check mfumo wa rejeta inaweza kuwa imeziba labda au check kama maji kwenye rejeta yamechanganyika na oil basi engine lazima ushushe
 
Nashukuruni kwa ushauri wakuu.

Nitafanyia kazi,

Ila wengi walishauri kwa kuchemka ni gasketi inahitaji rekebishwa
 
Nashukuruni kwa ushauri wakuu.

Nitafanyia kazi,

Ila wengi walishauri kwa kuchemka ni gasketi inahitaji rekebishwa
Yes. Ila kwa vile gari ni ya zamani, wakifungua kubadilisha gasket lazima wakute shida nyingine, so overhaul itakuwa pale pale. Na mie naungana na walioshauri utafute engine nyingine.

Shida kubwa kwenye overhaul ni mafundi na aina ya spare parts tunazotumia ambazo sio genuine.
 
Nilifanya overhaul, kabla ya overhaul niliomba ushauri kwenye uzi mmoja wapo hapa JF.

Wengi walisema usifanya nunua use. Wachache waliunga mkono. Siku nilipokuwa tayari nilienda Ilala kutafuta used nikiwa na fundi.

Kuna mambo kadhaa nilikutana nayo ambayo walipitiliza budget yangu, engine ilikuwa pouwa within budget.

Nikachukua maamuzi magumu ya kufanya overhaul ila nilikuwa mkali sana kwa fundi. Na nikafwatilia kila siku hatua anazofikia na naingia hadi google na youtube.

Leo nina engine 1JZ GTE ambayo imefanyia overhaul na ni kinanda, jino moja, ina nguvu hatari. Mwezi huu ni wa nne sasa no tatizo.

Ushauri wangu...Kama unataka engine nunua fasta.

Kama unaona budget yako inatosha overhaul, maana overhaul unafanya kwa engine ambazo ni complicated kupatikana. Tafuta fundi mzuri sana. Msimamie kila hatua. Usimpe usingizi maana hao jamaa ukijiachia tu utatoa hela na utachukua engine yako na kuiweka nyumbani.
 
Back
Top Bottom