Kufanya Uamuzi Makini.

Sosoma Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2020
Posts
312
Reaction score
281
Unapaswa kufanya nini unapopaswa kufanya uamuzi mzito?

Paula Cristina Ghibut alihitajika kufanya uamuzi mkubwa. Alikuwa na umri wa miaka 14, naye alikuwa mbioni kumaliza darasa la nane nchini Romani. Ilimpasa aamue ni wapi aende kuendelea na elimu ya sekondari.

Paula alitaka kuwa mwalimu wa shule ya msingi. Angeweza kwenda kwenye sekondari ya serikali yenye mchepuo wa ualimu lakini yeye tangu chekechea amekuwa akihudhuria shule ya Kiadventista. Na sekondari ya Waadventista hutoa mchepuo wa Sayansi.

Paula aliomba na kusoma Biblia nyumbani huko kijijini mwake Tagu Mure kaskazini mashariki mwa Romania. Aliongea na wazazi wake na kusoma aya kadhaa kutoka kwa kitabu kilichoandikwa na mjumbe wa Mungu Ellen White.

Kadri alivyosoma aligundua alipata aya zenye kuashiria ni vyema watoto wa Kiadventista wasome shule zisizo za Kanisa ili wapate kuwa na nuru ya ulimwengu.

Katika kitabu cha "Mashauri kwa Wazazi, Walimu, na Wanafunzi,'' alisoma dondoo hii: " Wafuasi wa Kristo wanapaswa kujitenga mbali na ulimwengu katika kanuni na mivuto, ila haipasi wajibague na kuishi peke yao mbali na dunia" (UK. 323). Katika Kitabu cha "Pambano Kuu" aligundua kuwa wanafunzi Wawaldensia waliposoma kwenye shule zisizo za kanisa waliishi kiinjilisti wakileta badiliko la kiroho katika shule hizo walizosoma mnamo karne ya 13 na baada ya hapo.

Hivyo Paula akashawishika kujiandikisha kwenye shule za jamii, akijiaminisha kuwa hiyo ni fursa kwake kumshuhudia Yesu kadri anavyojiandaa kuwa mwalimu.

Lakini alihitajika kwanza kushinda mtihani wa kujiunga na shule hiyo ya sekondari ya serikali. Akaomba, "Ee Mungu, ikiwa ni mapenzi yako nisomee hapo, niwezeshe nifanye vizuri."

Ushindani ilikuwa mkubwa mno. Kulikuwa na nafasi 150 tu shuleni hapo. Wanafunzi walioomba walikuwa mara nne zaidi ya nafasi hizo zilizopo. Hata hivyo Paula alipata ushindi wa juu mno mtihanini akashika nafasi ya saba kati ya hao 150 waliopata bahati kuchaguliwa.
Licha ya ushindi huo Paula bado hakujisikia amani. Ilikuwa vigumu kuachana na shule ya Kiadventista. Anajua shule za serikali hakuna maombi.

Wala fursa ya wanafunzi kumwimbia Yesu.
Majuma mawili kabla ya shule kuanza, Paula alipata ndoto kuwa ameshajiunga kwenye shule hiyo ya serikali. Walimu walijawa kiburi na chuki, wakawa wanamlaumu kwa makosa ya wana darasa wenzake. Shutuma hizo zilimkosesha raha Paula. Mwishoni mwa siku, alivyokuwa anajiandaa kwenda nyumbani, alisikia sauti ikimwambia. "Kimbia, Nenda zako, toroka, usirudi hapo shuleni tena!"

Alivyoamka asubuhi, alishangaa ndoto hiyo inamaanisha nini? Hakuwa na hakika ndoto hiyo inatoka kwa Mungu kwa vile alijua yule mwovu pia huleta ndoto. Aliomba "Ee Mungu, endapo ndoto hii inatoka kwako, ithibitishe kwangu kupitia njia nyingine."

Paula aliwageukia wazazi wake kuomba ushauri. Walimwambia anapaswa kufanya uamuzi wake binafsi. Hivyo alifunga na kuomba kwa siku kadhaa. Pia alisoma sana kutoka katika Biblia na kitabu cha Roho ya unabii. Alishangaa kuona kila kitu alichokisoma kilikuwa kikimwelekeza kwenda shule ya Kiadventista.

Katika kitabu cha "Mashauri kwa Wazazi, Walimu, na Wanafunzi," alisoma hivi: "Kuwakabidhi vijana wadogo wasome chini ya uangalizi wa mwalimu mwenye kiburi na jeuri ni jambo ovu." (UK. 175). Katika kitabu hicho hicho alisoma pia kuwa, "Shule za kanisa zimeamuriwa na Mungu kuwaandaa watoto kwa ajili ya kazi kubwa" (UK. 176).

Hivyo akafikia uamuzi, "Nilitaka kuanza maandalizi ya kuwa mwalimu kwa kujiunga katika shule ya serikali, lakini nimegundua shule ya Kiadventista itakuwa bora zaidi, japokuwa mchepuo wake ni wa sayansi."

Katika kitabu cha "Malezi ya Watoto" tunasoma, "Katika kujali elimu ya watoto nje ya nyumbani, wazazi yawapasa kutambua kuwa siyo salama tena kuwatuma shule za serikali, bali yawapasa kuwatuma kwa shule ambazo watapata elimu iliyojengwa katika misingi ya Maandiko" (CG, UK. 304).

Paula alienda kusoma shule ya Kiadventista. Paula alijifunza masomo muhimu katika kujua mapenzi ya Mungu. Aliomba na kuwauliza wazazi ushauri. Alisoma Biblia na Maandishi ya Ellen White. Ndipo hatimaye akafanya uamuzi. Paula ana hakika kuwa uamuzi alioufanya ni sahihi.

Wakati akiwa kwenye shule hiyo ya sekondari ya Waadventista, alijitoa maisha yake kwa Yesu na kubatizwa (soma Luka 4:16 na Matendo 17:2-3; 16:13; 13:42, 44 na Isaya 66:22-23) akiwa na umri wa miaka kumi na sita. Kwa sasa ana umri wa miaka kumi na nane na atahitimu hivi karibuni. Anajua kuwa atakuwa na muda wa kutosha kujifunza taaluma ya ualimu atakapokuwa Chuo Kikuu.

"Safari yangu ya kiroho imekuwa hatua kwa hatua," anasema Paula. "Sijawahi kutumia madawa ya kulevya na kisha kuwa na uongofu wa mwujiza. Badala yake Mungu aliniongoza hatua moja hadi nyingi ya ukuaji kiroho.

Napenda kuwatia moyo vijana wapate pia kuishi wakipiga hatua moja baada ya nyingine ya ukuaji kumfahamu Kristo zaidi na Neno lake. Katika kila hatua maishani mwetu, yatupasa tumtambue Yesu, naye atatenda kazi ndani ya maisha yetu.

Asanteni sana na barikiweni nyote!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…