Kufanyike uhakiki wa Deni la Taifa

Kufanyike uhakiki wa Deni la Taifa

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya miundombinu ikiwemo ya reli ya kisasa ya SGR, ujenzi wa bwawa la umeme la Nyerere na barabara za mwendokasi kutoka katikati ya mji wa Dar es Salaam kwenda Mbagala.

Hata hivyo serekali ya Rais Samia imeweza kupata mikopo mingi yenye riba nafuu kutoka Benki ya Dunia na Shirila la Fedha Duniani (IMF) ambayo mtangulizi wake. Mikopo hii inazidi kiasi cha dola za kimarekani 2 bilioni (zaidi ya Shilingi 4 trilioni) tangu Rais Samia aingie madarakani mwezi Machi 2021. Mikopo hii ambayo ilielekezwa kwenye shughuli za kukuza uchumi na kuboresha huduma za jamii ingetosha kabisa kuleta ahueni kwenye deni la taifa badala ya kuliongeza kwa kasi kubwa hivyo.

Kwa namna yoyote ile maelezo ya kina kutoka serikalini yanahitajika. Serikali ya Tanzania ni lazima ieleze ni kwa nini deni la taifa limeongezeka kwa kiasi cha Shilingi 20 trilioni ndani ya miezi sita. Hakuna mtu nje ya serikali, hata angekuwa na utaalam kiasi gani, ambaye angeweza kuelezea ongezeko kubwa kiasi hicho.

Dk Nchemba ni mwanasiasa. Inawezekana kuna baadhi ya taarifa ambazo hajazipata kuhusu ongezeko kubwa hilo la deni la taifa. Ni wakati sasa kwa Gavana wa Benki Kuu na wataalam wake kujitokeza kutoa ufafanuzi wa kina.
 
Back
Top Bottom