mwakavuta
Member
- Sep 22, 2020
- 99
- 306
Wakuu habari? Nina imani wiki imeanza vyema kwenu.
Nimekuwa nikijizuia kuleta hii mada hapa kwa muda mrefu lakini nakosa amani sana.
Kuna tatizo linakuja huko mbeleni kwenye majengo kama hayatatuliwa mapema.
Kwenye harakati zangu za kutafuta maisha kama kibarua wa ujenzi nilikutana na hali iliyonipa mashaka ya usalama kwenye jengo linalotumiwa na watu zaidi ya mia mbili sehemu mojawapo niliyofanya kazi.
Jengo la ghorofa 4 limekatika nyufa kubwa nyingi mno kazi yetu ilikua ni kuziba nyufa hizo. Kwenye uchunguzi wangu nilikuta yafuatayo,
* Nondo za nguzo za jengo zimeoza kwa kutu kiasi ukipiga tindo kidogo tu inakatika nyingine zimeisha kabisa.
Kuna sehemu ilibidi kukata ngazi maana imeoza kabisa na kuotesha nyingine.
* Nguzo zimekatika nyufa kuanzia ground floor mpaka floor ya nne juu, tunajua nguzo ndizo uti wa mgongo wa gorofa, kwa hali niliyoiona pakitokea mtikisiko kidogo jengo litakuwa chini.
Zimetumika kokoto nyeupe za uswahilini sio nyeusi ambazo ni imara zaidi. Sijajua tatizo lilikuwa ni nini "inawezekana walitumia maji ya chumvi kuchanganya zege ndio sababu ya kuozesha nondo".
NB: Sina uhakika kama wataalamu wa majengo walishirikishwa kutoa maoni yao juu ya aina ya marekebisho hayo, lakini kwa upande wangu njia pekee ya kutatua tatizo ilikua kubomoa jengo lote lisitumike zaidi ya miaka kumi.
Naomba kuwe na Sera ya ukaguzi wa wa usalama wa haya majengo kila baada ya muda, tatizo likitokea yatakua maafa maafa makubwa.