Kufaulu mitihani vizuri sio ‘kipaji maalumu’

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
24,225
Reaction score
22,632
Kuna huu utaratibu uliozoeleka kwamba watoto wanaofaulu vizuri mitihani yao ya kuhitimu darasa la saba na kidato cha nne huchaguliwa kujiunga katika shule zinazoitwa “Shule za Watoto Wenye Vipaji Maalum”. Baadhi ya shule hizi ni Ilbouru, Mzumbe, Msalato, Tabora, Kibaha na Kilakala. Kila siku nimekuwa nikijiuliza: ni vipaji gani walivyo navyo hawa watoto wanaochaguliwa kujiunga na shule hizi? Hivi kumbe kufaulu mitihani vizuri ni “kipaji maalum”? Je, ni kweli kwamba hizi ni shule za watoto wenye “vipaji” maalum? Na ni vipaji gani hivyo?

Nijuavyo mimi kipaji maalum ni kama vile kipaji cha ufundi, kusakata mpira (soka), kutunga, kuimba au kucheza muziki; ushonaji, useremala, uashi, uchoraji, ubunifu wa mitindo ya mavazi, n.k. Nitajitahidi kueleza. Kwa mfano, kuna wachoraji ambao akikuangalia mara moja tu, anaweza kukuchora sura yako kama ulivyo bila kukosea. Hawa wana kipaji maalum cha kuchora. Sio kila mtu anayeweza kuchora kwa ufasaha hata kama akiigilizia kitu anachokichora. Ikiwa huwezi kufanya hivyo, basi ujue kwamba huna kipaji cha kuchora.

Katika nchi zilizoendelea, watoto wenye vipaji kama hivi hugunduliwa mapema na kutengewa shule maalum ambazo hutumika kuendeleza vipaji vyao. Wengi wa wanasoka wanaosifika ulimwenguni wana vipaji vya kucheza mpira. Vipaji vyao vilionekana tangu wangali wadogo na vikaendelezwa. Kufaulu vizuri masomo sio kuwa na kipaji maalum. Serikali imeshindwa kuibua au kugundua vipaji vya watoto na kuviendeleza, badala yake imekuwa ikiwahadaa wananchi kwamba kufaulu vizuri ndiyo kipaji maalum!

Kuna wagunduzi mbalimbali katika nchi hii ambao kama serikali ingekazana kuendeleza vipaji vyao tungeondokana, kwa kisasi fulani, na matumizi makubwa ya pesa katika kununua teknologia na kuajiri wataalamu kutoka nje. Katika miaka ya hivi karibuni, kuna mtanzania mmoja aligundua mashine ya kusaga nafaka ambayo hutumia nguvu za maji yanayotiririka. Mwingine aligundua teknologia ya kutengeneza ndege kwa kutumia vyuma chakavu na kufanikiwa kuirusha angani kwa dakika kadhaa. Na wa mwisho aligundua teknolojia ya kurusha matangazo ya redio. Endapo serikali yetu ingekuwa makini ingeviendeleza vipaji vya wagunduzi kama hawa na hatimaye tukaja kuwa na teknologia yetu sisi wenyewe ambayo baadaye tungeomba msaada kutoka nje tukaiboresha na kufikia teknologia kamili.

Uzoefu unaonesha kwamba wagunduzi wengi wa karne iliyopita hawakuwa na uwezo mkubwa sana darasani kama hawa vijana wetu “tunaowabatiza” kuwa “wenye vipaji maalum”. Mfano mzuri ni Bill Gates ambaye aligundua teknologia na matumizi ya kompyuta. Huyu mtu hakuwa mzuri sana darasani na inasemekana kwamba alikimbia shule (school dropout). Ila kwa kuwa serikali yake ilikiona na kukithamini kipaji chake, haikusita kukiendeleza. Hatimaye tumepata kompyuta, nyenzo ambayo imesaidia sana kurahisisha kazi za kila siku za mwanadamu.

Mpaka hapo nadhani tumeishaona tofauti kati ya kufaulu vizuri darasani na kipaji maalum. Hivyo basi, serikali iache kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa kwa kutuaminisha kwamba hapa Tanzania tunazo shule za watoto wenye vipaji maalum! Jibu ni kwamba hakuna shule hata moja ya aina hiyo katika nchi hii; badala yake tunapumbazwa bure kwa kuaminishwa kitu ambacho hakipo. Tija ya hizo shule (wanazosoma watoto waliofanya vizuri kimasomo) kwa maendeleo ya taifa, kama ipo, ni kidogo sana. Hazitoshi kuifanya serikali itoke kifua mbele kwa kutenga shule za namna hiyo. Wananchi tuweni makini na baadhi ya kauli za serikali. Akili za kuambiwa, tuchanganye na za kwetu!
 
Hoja yako sijaielewa vizuri ndugu yangu,lakini nia ya serikali ikuwa kuwatafuta watoto waliofaulu kwa alama za juu darasa la saba na form iv ili baadaye wawe wataalamu katika fani mbalimbali udaktari,uhandisi na uwanasheria na n.k na wakati hule wamafanikiwa sana.kwa mfano mimi nimesoma ilboru miaka ya 1997-2000 na nimebahatika kusoma na wanafunzi wenye akili nyingi ambao wana uwezo wa kupata A zote ambao wameenda katika vyuo vinavyoeshimika duniani kama havard,yale hongkong,denmark n.k.na wengine wamefanya kazi ktk taasisi za kimataifa duniani.nakukaribisha tunapage ya ilboru facebook uje ufanye utafiti kidogo.kuhusu suala la ugunduzi sidhani kama ilikuwa nia ya special schools.
 

Siku hizi zinaitwa "Special School" na Si hizo za vipaji maalumu ila all in all wengi wapo juu sana hata kimaisha ya mtaani
 
Ila ni kweli kuna watu wanavipaji kwenye hizi shule ila wengine ni wa kawaida sana
 

Unawezaje kuthibitisha kwamba wahitimu wa shule za 'vipaji maalumu' wameleta manufaa kwa taifa la Tanzania?
 
Ila ni kweli kuna watu wanavipaji kwenye hizi shule ila wengine ni wa kawaida sana

Kufaulu vizuri masomo kunategemea mambo mengi, ikiwemo mazingira ya kusomea, uwepo wa walimu wa kutosha na wanaojituma kufundisha, na sababu nyingine nyingi tu.

Kusema kwamba wanaofaulu vizuri wana 'vipaji maalum' ni kutokujua maana ya neno 'KIPAJI'. Kama kufaulu tu ni kipaji, basi wote wanaofanya vizuri wana 'vipaji maalum'!!!!!!!
 
-kwahiyo kuwa daktari au mwanasheria ndio unakipaji maalum?

-kwahiyo kusoma havard au mit nchi za nje ndio una kipaji maalum?, -kwahiyo kupata A masomo yote ndio kipaji maalum?,anaepata A somo moja je?, kipaji maalum kwako unaelewa nini pamoja na kusoma shule hiyo mnayoiita ya vipaji maalum?
 
Hehehe vipaji maalum...a funny term,sijui ata walimaanisha nini..na me nilisomaga shule ya kipaji maalum aisee...it was nice though
 
Ukiwa kilaza afu ukaongeza na chuki bila kusahau roho mbaya ndo utapata mawazo kama ya huyu mleta mada, mie ckubahatika pita huko bt kiukweli nawapa hongera wote wenye vipaji maalum hata kufaulu sana pepa n kipaji pia y yeye apate A afu ww upate D akat mwal n mmoja na darasa n moja? Learn to appreciate mleta uzi


Sent from my iPhone using JamiiForums.🔩🔨
 
Hivi unadhani kufundishwa/kusoma, kuelewa na kufaulu vyema sio kipaji.?

Kuelewa ni kipaji, kucheza mpira ni kipaji, kucheza shoo ni kipaji. Tatizo kubwa ninaloliona hapa ni mfumo wa tanzania kuwa mbovu, vitu havifuati proffesionalism, proffessionals hawathaminiwi katika fani zao na wako underpaid zaidi ya wanachokifanya huku watu wa hovyo wakipata pesa nyingi kwa shortcut kama vile (madawa ya kulevya, wizi/ufisadi, rushwa, kujuana etc).

Mind you siku hizi ni wanafunzi asilimia chache sana utakaowaambia habari za kusoma can make you having good life wakakulewa. Wengi akili zao zimekuwa filled na ujanjaujanja na shortcuts kama silaha ya mafanikio. Wizi/deal umekuwa kitu cha kujisifu katika tanzalnia ya sasa. How come mtu aje kuona kufaulu sana ni kipaji ilhali amemzidi mafanikio au wanalingana yule alofaulu sana.

So ni system ya nchi ndio mbovu/ these guys walofauli sana ndio ilitakiwa wawe think tank. No wonder nchi inaenda hovyo kwa kutojali hili. Waziri wa elimu(mulugo) alipata 0 na kafoji vyeti, unategemea nini katika elimu ya nchi.?
 
Hivi unadhani kufundishwa/kusoma, kuelewa na kufaulu vyema sio kipaji.?

Kufaulu vyema pekee siyo kipaji maalumu bana.

Mtu unaweza kabisa ukawa na average intelligence lakini ukawa na juhudi za kujisomea pamoja na mbinu za kusoma yale yaulizwayo kwenye mtihani na ukafaulu vizuri tu.

Ila kwa nchi kama Tanzania, yenye viwango vya chini karibu katika kila kitu, sishangai kwa nini mtu anayefaulu mitihani ya mwisho kuonekana ni mwenye kipaji maalumu.
 
hoja ya mtoa mada anajaribu kuangalia kama ni kweli hizi shule za vipaji maalumu zinabeba uhalisia wa vipaji maalumu, of which is A BIG NO. matokeo kuwa mazuri haimaanishi kipaji maalumu, kipaji maalumu is a very unique thing, and is when we come up with memorable people in a specific area when talking of a talent, siku hizi hizo shule zenyewe hizo hata kumi bora haziingii kama mwaka jana zilianzia 40, sasa ndo tuseme vipaji maalumu zimekuwa private? we cant say so, just a process can make students perform marvelously but no way can someone inculcate talent to anyone. huo ndio ukweli
 

you nailed a point, kwa leo sitakuwa na mengi ya kusema unless nichokozwe lakini haya maelezo yanatosha na inabidi hizo shule zifanyiwe mabadiliko makubwa ili kuendana na majina yake pamoja na kusudio lake
 
Alaaa! Kumbe nawe una kipaji maalum? Hongera zako!

ahsante japo kiuhalisia, mi hata sijaona anything peculiar from that school,hakuna cha kipaji cha aina yoyote aisee masomo tulisoma kama wa shule zingine tu,labda ni vile tu zina walimu kuliko shule za govt zingine na wanachukua passmark kubwa kdogo,juhudi binafsi tu ndo zitakusaidia mana hapo hapo shule tulitoka primary vipaji maalum wote form 4 wengine wanatoka na div 0 wengine 1..
Afu sikuhizi zimechujaaa mbayaa
 
Wametoka darasa la saba wamefaulu vema wakarundikwa seheme wakatengenezewa mazingira mazuri i.e maktaba, maabara, walimu, misosi na mabweni kushinda wengine afu unawaita wana vipaji maalumu kwa kupata A nyingi, mi sikubaliani na hilo wenye vipaji ni wale waliotoka na ufaulu wa kawaida shule ya msingi wakaenda sekondari za kawaida zenye hadhi ya shule za mkapa(kata) wakafaulu kwa kupata A za kutosha
 

Na wale wanaoiba paper wakapata divisheni wani na kuchaguliwe kwenda Ilbouru wana kipaji cha KUIBA PAPER au kipaji maalum?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…