50/250=1/5=20% ndiyo ya kujiunga na form 1?Kichekesho cha mwaka,mbaya zaidi hizo 20% zinaweza kuwa za kudesa au saidia ufaulu wa shule.Wakati hule mie naingia form 1 yalikuwa masomo matatu kwa 50 maks kila somo=150 na kufaulu ulitakiwa mvulana kuanzia 80 maks na waschana 70/75 lakini leo masomo 5 =250maks lakini cha ajabu watoto wanapelekwa form1 kwa maks below 50
hapo ndo hesabu inapogoma kuingia kichwani kama Tanzania tuna elimu ama tuna watu wanaoingia na kushinda madarasani na kbaya kuliko vyote ni pale unapowakuta hawa wanaopelekwa darasani kwa ufaulu wa 1/8maks wanahudumiwa na walimu wasiozidi 3 shule nzima...huwa najikuta nashikwa na tumbo la kuhara
Mimi naona Tanzania sahv elimu imetushinda na tunachokfanya ni kujarbu ujinga,ngoja tuone mwisho wake nini.
HAHAHAA! hukuweza hata kuibia kwa jirani yk?Kumbe ndo maana sikupasi la saba!
.Ndio maana wazazi wenye nazo wanawapeleka watoto wao private schools ambako hata mtihani wao wa kujiunga ni mzito kuuzidi huo wa serikali.
sijaelewa hapo. Kwani mtihani wa darasa la 7 kuingia form one unatofautiana kati ya shule za serikali na binafsi au?
Kweli mkuu.Tatizo ni sera mbovu za elimu zinaondeshwa na nchi, zimejikita zaidi katika kuangalia quantity of education inayotolewa na sio quality of education provided na tukiendelea kuendesha elimu hii kisiasa zaidi tutaendelea kuwa na wahitimu wa hadi kidato cha nne wasiojua kusoma wala kuandika, inashangaza kuona mwanafunzi yuko sekondari lakini hajui kusoma wala kuandika, kazi kwa wadau wa elimu, viongozi wetu hawana uchungu na elimu, watoto wao wako wapi? "Ukitaka kuona utamu wa ngoma cheza" je wao hucheza nasi?