Kufeli ndiyo mwanzo wa kufanikisha jambo na sio mwisho wa jambo

Kufeli ndiyo mwanzo wa kufanikisha jambo na sio mwisho wa jambo

badshah

Member
Joined
Mar 16, 2013
Posts
51
Reaction score
32
Watu hawatafikiria vibaya endapo utafeli, huenda watu wakakushangaa kwa kule kutojaribu mbinu za kufanikisha ndoto zako. Ukweli ni kwamba, watu hao watakuheshimu kwa kujaribu kwako.

Kitu kikubwa ambacho watu wanaweza kukuweka katika fungu baya ni ile hali ya kujinyongesha na kuonekana dhaifu pale unapofeli. Kumbuka kuwa kufeli sio mwisho wa jambo bali ndio mwanzo wa jambo na ni changamoto kubwa sana katika mafanikio. Na katika hofu kubwa sana ambayo inatakiwa iogopewe ni kwamba ulimwengu wako mzima utaanguka pale utakapofeli.


Ukweli ni kwamba hutokea kwa nadra sana, muda mwingi unatakiwa kurudia jambo ambalo unahisi umefeli nalo, kwa kurekebisha sehemu mbalimbali ili uweze kuwa katika njia iliyo nyoofu kabisa kwani huenda hapo mwanzo kuna baadhi ya vitu vichache tu ambavyo ulikuwa hukuviweka sawa. Na ndio maana ikasemekana kuwa kufeli ni mwanzo wa kutengeneza jambo vizuri.

Hebu fikiria kuwa umefanya kitu ambacho hakina mkosoaji, na siku zote nafsi yako huridhika na jambo unalolifanya kwani ndiyo mahitajio yake. Hivyo kama hakuna mtu atakayekukosoa au kukupa ushauri wa jambo lolote lile basi unaweza kuona uko sahihi kabisa, huenda ikawa kweli lakini pia uhakika bado ni asilimia ndogo.

Ili uweze kufamikiwa katika jambo lako ni vema utake ushauri nalo na uwaonyeshe watu kazi yako usikie maoni yao juu ya kazi yako, na wanapokukosoa ndio iwe furaha yako kwani ndio unapozidi kuweka marekebisho na kuboresha kazi yako.

Watu wengi hukasirika sana wakikosolewa au kufeli kwa jambo bila ya kufahamu kuwa hiyo ndiyo njia sahihi ya kutengeneza jambo lako na kufanikiwa nalo katika maisha yako. Utakuta mwanafunzi akifeli katika masomo yake hukata tamaa kabisa na wengine hata kuamua kujiua, lakini hebu jiulize juu ya watu wenye nafasi nzuri ulimwenguni, angalia historia zao za masomo hapo nyuma au hata kama sio masomo basi hata kwa kazi zao za nyuma, utaona walipata changamoto kubwa sana hapo nyuma, walihangaika, wengine walifeli na kujitahidi kurudia mara nyingi kwa kurekebisha makosa ya nyuma, wngine walitaka ushauri kwa wenzao kuhusu kazi zao. Na mpaka sasa hufaidi matunda ya uvumilivu wao.

Staryte - Elimu, Burudani na Maendeleo

Huu ni mwanzo sasa, hakuna haja ya kuanguka katika njia ambayo tayari umeshaishika, kwahiyo unaweza kutekebisha kidogo baadhi ya makosa katika safari yako mpya. Kitu kikubwa ambacho unatakiwa kuepukana nacho ni uoga wa kufeli. Hakuna haja ya kuogopa kwani kuna msemo unaosema kuwa "hatuna haja ya kuogopa bali tuogope kuogopa” na hii ni kweli kwani uoga wa kutarajia kufeli ni mkubwa kuliko ule ambao umeshajitokeza kwa kufeli.
Hivyo basi kujiingiza katika hofu na kuacha kujaribu, unajiweka katika mambo mabaya na kukosa mafanikio, hivyo anza kujiambia mwenyewe kuhusu mambo mazuri! Badilisha muelekeo wa fikra zako na anza kuona uwezekano wa mafanikio, sio kufeli. Kumbuka, kuwa kufeli kunaweza kukusaidia katika kutengeneza mafanikio ya baadaye.
 
ongeza na sentensi hii kuwa kwenye nukta haimaanishi ndio mwisho wa habari kwani bado unaweza kuanza sentensi nyingine hata baada ya nukta.
 
Back
Top Bottom