Kuficha mvi ni kumtegea nani?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,468
Reaction score
911,184
Wenye mvi tukubali ujana una mwisho na hivyo tuache kuhadaa vijana kuwa bado tumo wakati ni saa za majogoo......tuache kutia kanta vichwani ili tuonekane hatujazeeka kumbe masaa yameyoyoma...........hivi tunapohadaa jamii lengo ni kumtega nani?

ugonjwa huu zamani ulikuwa kwa akina mama lakini na akina baba tumeambukizwa.................utakuta watu wazima hawataki shikamoo ambayo ni dalili ya kuwa mtu mzima na ya kuwa jamii yakuona una busara sana........hivi wewe mwenye rangirangi kichwani unamtega mtoto wa nani na ili umfanye nini?

Grey hair: should I dye it?

Is it essentially compulsory for women to reach for the colour bottle when the grey starts to show?

Sex and the City's Carrie … how did she get that hair? Photograph: Bill Davila/Rex Features

I have started to notice some grey hair on my head. I don't mind but I have noticed that most other women all have perfect auburn hair, despite being my age or older. Is it now a given that I have to dye my grey?
Sonia, London
 
mimi najivunia mvi zangu sioni sababu ya kuzificha kwani nitakuwa ninajihadaa mwenyewe.............pili kwa wale ambao hawapendi ziwe nyingi jibu ni kula kwa kiasi na kufanya mazoezi................tumia njia za asilia badala ya madwa katika kupunguza kuzeeka kwa haraka.........haraka ambako husababishwa na mwili kukosa mazoezi au kuvimbishwa na milo kupita kiasi.......
 
Ndio maana unaanzisha mada na kujijibu mwenyewe. Nani alikwambia wanaweka peacock kujificha?

Mimi nafikiri ni suala la kupendeza. Na kwa taarifa yako kuna watoto wa umri wako wana mvi
 
Ndio maana unaanzisha mada na kujijibu mwenyewe. Nani alikwambia wanaweka peacock kujificha?

Mimi nafikiri ni suala la kupendeza. Na kwa taarifa yako kuna watoto wa umri wako wana mvi

Hivi ukiwa na mvi wachukiza!!!!!!!!!!!!!!! Mie ninazo kibao lakini naona niko fiti tu...na hao wanaona lengo ni kupendeza ili iweje?..............wanalenga kumvuta nani?
 
mkuu ruta mimi ndio nakaribia kugonga 30yr lakini nazipenda coz zilinianza tangu nikiwa form two.....problem which i face nikiwa nimekaa mtu akitokea kwa nyuma asipokuwa makini lazima anipe shikamoo kuna siku mke wa boss wangu kanipa shikamoo nikazuga kuipotezea palikuwa apatoshi the next day boss akaniuliza mbona uwa siwek super black.ninapenda kupokea shikamooo wala sijuti kuwa na mamviiiiii....
 
Sometimes mvi si uzee, zipo za ukoo na wakati mwingine ni kweli hu-reflect umri wa mtu. Ila sioni kama kuna tatizo kama mtu akiwa anajipenda akaamua kupaka hizo dawa za kufanya nywele ziwe nyeusi. Kujipenda hakumaanishi kuwa mtu unaficha umri.
Ila kwa wale wenye tabia za kuweka dawa kwa kuficha umri, hilo ni tatizo, wanapaswa kujirekebisha maana hizo ni dalili za uharibifu kwa vijana wetu.
 
Hivi ukiwa na mvi wachukiza!!!!!!!!!!!!!!! Mie ninazo kibao lakini naona niko fiti tu...na hao wanaona lengo ni kupendeza ili iweje?..............wanalenga kumvuta nani?

Kila mtu ana mtazamo wake na kupendeza ni utashi wa mtu kwa hiyo sijui wewe ni nani hadi watu wakitaka kupendeza waombe ruhusa kwako na watoe maandishi ya kuwa wanalenga kumvutia nani.

Kwani wewe unataka wasipendeze ili iweje?
 
Hivi mtu akiwa na umri mkubwa halafu wewe huujui, unaharibika eeh?

Hii kweli inaumiza mbavu. Yaani mtu akificha umri wake wewe kijana wako anaharibika, mweh!
 
Kila mtu ana mtazamo wake na kupendeza ni utashi wa mtu kwa hiyo sijui wewe ni nani hadi watu wakitaka kupendeza waombe ruhusa kwako na watoe maandishi ya kuwa wanalenga kumvutia nani.

Kwani wewe unataka wasipendeze ili iweje?

mbona unakwepa kujibu swali.......itabidi nilirudie...................ukiwa na mvi hupendezi?
 
upo uhusiano wa moja kwa moja kati ya ufataki na kuukataa umri...........lengo ni kuwahadaa wale wenye umri mdogo waone ya kuwa kumbe nawe bado wamo.....................kumbe tayari umekwisha kukongoroka........
 
wahahribifu wa mazingira utawaona tu.............ni vigumu kujificha.......

Unajua wewe unashangaza sana! Hebu nijibu haya maswali yangu bila unafiki wala kuleta kujua:
Hivi nyumba yako inapokaa miaka mingi mpk rangi zikafubaa na ukaamua kuipaka rangi, pengine na kubadili nyavu za mbu n.k (renovation)
1. Unaipaka rangi ili iweje?
2. Kama jibu la swali la kwanza ni IPENDEZE, je unataka ipendeze ili iweje?
3. Kwani nyumba yenye rangi za kale na ukungu ni mbaya?
4.Unaipaka rangi kumdanganya nani kuwa ni mpya?
 
tuko wachache kwenye hili kundi...................ni nija nyembamba sana hii na wengi wanapenda ile njia pana......
 
Mbona sio mvi peke yake zinazonyesha kua huyu jamaa ni mzee,labda wanaume wengine wanaona haya mvi lakini mie sioni mvi ni aibu kwa mwamume au tatizo lininyime raha ya kula vyangu...
 
mbona unakwepa kujibu swali.......itabidi nilirudie...................ukiwa na mvi hupendezi?

Nilishakujibu kuwa kupendeza ni mtizamo wa mtu. Wewe unaweza kuona unapendeza na mvi mwingine akaona hapendezi.

Na kama kupendeza kwako siyo ishu, mbona uliuliza kama ukiwa na mvi unakuwa hujapendeza? Wewe umeona mvi zinakupendeza sasa juu ya nini uulize wenzako wanataka wapendeze ili iweje
 
mwanadamu siyo nyumba...................ukarabati wa mwanadamu ni chakula na mazoezi siyo kujipakaa poda klichwani lol..................kubwa zaidi naona nimekukamata pabaya leo...........
 
upo uhusiano wa moja kwa moja kati ya ufataki na kuukataa umri...........lengo ni kuwahadaa wale wenye umri mdogo waone ya kuwa kumbe nawe bado wamo.....................kumbe tayari umekwisha kukongoroka........

Kwa hiyo hapa unawaza kutongozwa au?

Hivi binti yako akitongozwa na kijana unapata faida gani ambayo akitongozwa na mzee utaikosa? Mi nilidhani suala ni binti yako kuwa makini na wazee na vijana!
 
mwanadamu siyo nyumba...................ukarabati wa mwanadamu ni chakula na mazoezi siyo kujipakaa poda klichwani lol..................kubwa zaidi naona nimekukamata pabaya leo...........

Huna hata robo ya ubongo wa kukuwezesha kunishika pabaya.

Hapa hatuzungumzii ni ipi njia bora ya kukarabati nyumba au mwili, mada yako ni UKARABATI UNAFANYWA ILI KUMDANGANYA NANI.

Well then, kama nikila hicho chakula bora na mazoezi nikazikwepa mvi, umeshapata jibu nitakuwa namdanganya nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…