cold water
JF-Expert Member
- Oct 6, 2021
- 238
- 954
Let s say unaenda sehemu fulani ni ugenini na hiyo sehemu unayoenda inaweza kuwa na ndugu zako au marafiki vipi ni bora ufikie guest au kwa ndugu? Hilo ni swali sasa twendeni kwenye point au ujumbe niliotaka ku-share hapa.
Nilisafiri last month kutoka mkoa ninaoishi kwenda mkoa fulani, nilifikia kwa rafiki jamani nilitumia gharama nyingi nikajisemea moyoni bora ningefikia guest
Nilivyofika tu ile siku ya kwanza kunipokea nikampa elfu tano kama matumizi aongezee kwenye suala la chakula, nimefika kwake kama leo, kesho yake akanambia sina vitu ndani (chakula) twende town, nikamwambia sawa.
Anapoishi ni mbali kidogo na mji japo sio sana ni kama dk 10_15, ukipanda boda boda. Katika hiyo safari cost zilivyoanza sasa tukapanda boda hadi sehemu Fulani, muda wa kumpa nauli boda boda sasa, friend akatoa elfu kumi boda akasema sina chenji, rafiki yangu akaniuliza huna ela ndogo hapo nitakurudishia, kweli nilikuwa nayo ela ndogo nikaitoa,ilo likapita
Tukaenda tena sehemu fulani kununua maji kwenye dumu kubwa la lita 10, akatoa hela muuzaji akasema hana chenji, friend akaniuliza tena huna ela ndogo hapo nitakupa nikatoa tena. Sokoni sasa kufanya hiyo shopping yake ya chakula kila ela anayotoa wauzaji hawana chenji mimi ndio nilikuwa na ela ndogo ndogo bwana nikajikuta nimetumia ela nyingi
Tulivyokuwa tunarudi tulipanda bajaji, anaambiwa nauli friend hana ela ndogo tena ikabidi niendelee kutoa zangu. Tumerudi home hakunipa zile ela mi nikampotezea wala sikumkumbusha.
Siku ya tatu nikasepa maana nilikaa siku tatu tu.
Kisa cha kwenda kwa rafiki ni hiki mkoa huo huo kuna ndugu yangu kiukoo ila sio ndugu kivile alinipokeaga Mara ya kwanza before sijafikia kwa friend, ndugu yangu alipika chips muda wa kunisevia chakula akawa anatumia mikono, yaani zile chips anazichota kwa mikono kama kijiko ivi huku naona na bwana ake anamuangalia tu, bwana ake ndo ndugu yangu mimi, nyama ya kuku alikaanga kavu, nayo akawa ananitilia kwa mikono, though nilikula hivyo hivyo kwa kujikaza lakini kitendo hicho hakikunifurahisha ndo maana awamu ya pili nikaamua kufikia kwa rafiki angu, coz niliona guest gharama japo maisha ya guest ni ya ku-relax sana.