SoC04 Kufikia mapinduzi makubwa ya kisayansi

SoC04 Kufikia mapinduzi makubwa ya kisayansi

Tanzania Tuitakayo competition threads

carlmax II

New Member
Joined
Dec 31, 2021
Posts
4
Reaction score
2
KUWEKEZA KWA WALIMU WA MASOMO YA SAYANSI NA HISABATI ILI KUFANYA MAPINDUZI YA SAYANSI.

Kufanya mapinduzi ya Sayansi na teknolojia serikali inapaswa kuwekeza kwa Walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati ili kuongeza msukumo na kuendana na kasi ya dunia kwenye matumizi ya sayansi na teknolojia kwenye nyanja mbalimbali kama vile elimu, Afya, ulinzi, viwanda, miundombinu na biashara.

Upungufu mkubwa wa walimu wa masomo hayo kuanzia shule za msingi hadí vyuoni, inapelekea kuzalisha wataalamu wachache wa sayansi na teknolojia ikiwamo na walimu wa masomo hayo ambayo in Kemia, Baílojia, Fizikia pamoja na Hisabati. Ili kuondoa kabisa tatizo hilo Serikali iwekeze Fedha nyingi kwa walimu kama inavyowekeza kwenye miradi mikubwa na miradi ya kimkakati.

HATUA ZA KUCHUKUA.
Kwanza serikali ibadilishe muundo wa mishara ya walimu wote (TGTS scale) na kupandisha hadi Kima cha chini cha mshahara wa Mwalimu yoyote kiwe sio chini ya Tshs 800, 000/= kwa walimu wa masomo yote kuanzia ngazi ya elimu ya astashahada (diploma), Ualimu ngazi ya cheti ufutwe.

Pili ianzishwe Posho ya Kufundisha masomo ya sayansi kati ya 30% hadi 40% ya mshahara wake kulingana muda kazini, Pamoja na ngazi ya mshahara. Walimu wa sayansi wakiwa na mshahara mzuri na malupulupu itaboresha maisha yao, maisha yao yakiboreka watatekeleza majukumu yao kwa utulivu na umakini. Lakini pia maisha bora kwa walimu yatawashawishi hata wanafunzi wao watamani kusomea na kutamani kufanya kazi ya Ualimu muda wao ukifika.

Pia kwenye shule za pembezoni haswa haswa vijijini Serikali ijenge nyumba za walimu wa sayansi na Hisabati kwenye shule zote za msingi na zile za sekondari. Hizo nyumba ziwe maalum kwaajili ya walimu hao, hatua hiyo itapunguza tabia za walimu wa sayansi na hisabati kuyakimbia maeneo ya pembezoni na kukimbilia shule za mijini.

MATOKEO TARAJIWA.
Hii itasaidia walimu wa Sayansi kutumia muda zaidi kuandaa masomo na na majaribio (activities) ari ya wanafunzi kwenye masomo haya itaongezeka zaidi na Kuongeza idadi ya wanafunzi wataochagua (kuopti) kusoma masomo hayo kuliko sasa. Idadi kubwa ya wanafunzi wanafanya masomo ya sayansi kutaongeza idadi ya watahiniwa pamoja na kuongeza idadi ya wanavyuo wanasoma kozi za masomo ya sayansi.

Ufaulu pia utaongezeka na kumaliza kabisa upungufu wa walimu wa masomo hayo ndani ya miaka mitano hadi kumi. Walimu wa sayansi wanamzigo mkubwa sana wa vipindi vya kufundisha kutokana na uchache wao, hii inasabisha ufaulu kwenye masomo ya sayansi na Hisabati kuwa chini mwaka hadi mwaka. Hii hatua itasaidia pia kupunguza uchache wa walimu hao.

Wanafunzi waliofanya vizuri sana masomo haya Watasomea fani nyingine kama utabibu, uhandisi, na ubunifu. Hii itawapa fursa nzuri za ajira ndani na nje ya nchi pia kufanya ubunifu na kuanzisha miradi kama viwanda na makampuni na kufanya wigo wa ajira nyingine na kuongeza pato la nchi.

Msingi mzuri wa sayansi ya kwa wanafunzi huzalisha wanasansi bora watakaoleta mabadiliko makubwa sana kwenye kila sekta kwa kutumia Sayansi na teknolojia. Teknolojia kwenye sekta kama madini, utalii na Afya itakuza makusanyo kwenye sekta hizo na kukuza pato la taifa maradufu na kupunguza utitiri wa kodi kwenye biashara nyingine na kuondoa malalamiko na migomo ya wafanyabiashara.

Teknolojia yenyewe pia ni bidhaa hivyo kuwekeza kwenye walimu na masomo ya sayansi kutachechemua uvumbuzi wa kisanyansi. Wale wavumbuzi watakuwa matajiri wakubwa wakiuza teknolojia zao kama ilivyo kwa bilionea Bill Gates mvumbuzi na mmiliki wa Microsoft. Kutokana na biashara zao kuwezesha serikali kupata mapato kutokana na kodi na tozo mbalimbali za mauzo ya teknolojia.

Teknolojia itawezesha Tanzania kutumia na kutunza rasilimali tulizobarikiwa kama bahari, misitu na madini. Rasilimali zitatumika nchini kuwanufaisha wananchi wote badala ya kusafirisha nje ya nchi kuongezewa thamani halafu tunauziwa tena kwa bei kubwa mno.

Sayansi na teknolojia ndizo zana za kurahisisha maisha ya mwanadamu. Tanzania kama nchi ili kuendelea kwenye teknolojia ni LAZIMA WALIMU WA MASOMO YA SAYANSI NA HISABATI KUWEZESHWA ILI NAO WAWAWEZESHE VIJANA KUWA WANASANSI BORA SIKU ZA BAADAE.
 
Upvote 4
Back
Top Bottom