Kufikia Mauzo ya Platnum

Kufikia Mauzo ya Platnum

barcelonista

Senior Member
Joined
Apr 26, 2021
Posts
158
Reaction score
149
Wakuu kwema? Tueleweshane kidogo kwa wale wanaofahamu.

Ni vigezo gani hutumika kuifanya nyimbo kuuza mauzo ya Platinum. Kwa mfano hii Essence ya Wiz Kid imefikisha Mauzo hayo ndani ya U.S.A Baada ya kuuza Units 1 Milion.

Na inaonekana sio rahisi kwa sababu huchukua muda ngoma kufikia mauzo hayo, na sio kila hit inaweza kuuza Platinum.

Hii imekaaje?



Screenshot_20210921-213952.png
 
Zamani kabla ya streaming hazijashika hatamu ilikua rahisi sana kujua mauzo HALISI maana nyimbo zilikua zinauzwa kwenye cd au kaseti au santuri au unadownload baada ya kuulipia

Lakini siku hizi ukilipia na ku subscribed labda Apple music au Tidal au Sportfy nk wimbo mpya ukitoka wewe kaZi yako ni kuwa na bando na kaustream tu

Hivyo basi kuna formula mpya ya kusema wimbo umefikia kiwango kipi cha mauzo
Sijafatilia sana ila wanachofanya ni kuchukua jumla ya streaming na wanazigawa kwa rate zao ili kupata equivalent to “pure sales” halafu ndio wanajua kama mauzo ni gold au platinum ama diamond
 
Back
Top Bottom