manssamussa
New Member
- May 2, 2024
- 2
- 1
Nchini Tanzania, hali ya umasikini bado imetamalaki licha ya jitihada mbalimbali kuchukuliwa ili kupunguza umasikini na kukuza uchumi. Jitihada za kupunguza umasikini zimeonekana kuwa na matokeo hafifu kutokana na ongezeko kubwa la watu. Hivi sasa Tanzania inakadiriwa kuwa watu zaidi ya milioni 26 ambao wanaishi katika hali ya umasikini uliokithiri. Pia, taarifa mablimbali zinaonesha katika kila watanzania wanne kuna watanzania watu hurudi katika hali ya umasikini uliokithiri japo walifanikiwa kuukacha umasikini. Hivi karibuni lilifanyika zoezi la sensa na lilionesha kuwa asilimia 68% ya watanzania wana umri kuanzia miaka 15 mpaka 35. Matokeo ya sensa yalionesha kuwa Tanzania ina kundi kubwa la vijana ambao ni nguvukazi ya kujenga na kukuza uchumi.
Licha ya kuwa Tanzania imejaaliwa kuwa na kundi kubwa la vijana ambao ni nguvukazi ya taifa, vijana wengi wamezingirwa na hali ya umasikini uliokithiri sambamba na ukosefu wa ajira. Lakini pia wanawake wanaonekana kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira kwani ripoti mbalimbali zinaonesha wanaume wana nafasi kubwa ya kupata ajira na pia hulipwa zaidi kuliko wanawake hata kwa kazi za ujuzi unaofanana. Ukiachana na vijana na wanawake, wazee na watu wenye ulemavu pia wako katika hatari kubwa ya umasikini uliokithiri unaochangiwa na kukosa fursa endelevu za ajira.
Katika muktadha huo, Tanzania inakabiliwa na jukumu kubwa la kutengeza fursa za ajira kwa ajili ya vijana, wanawake, wazee na wenye ulemavu (makundi maalumu). Katika kutambua umuhimu wa fursa za ajira kwa makundi maalumu tajwa, serikali imedhamiria kuhamasisha ujasiriamali na kutengeneza nafasi za ajira. Dhamira ya serikali kutengeneza fursa za ajira kwa makundi maalumu inaonekana pale ilipoamua kutumia nguvu yake ya kifedha/kibajeti ili kuwezesha kiuchumi makundi maalumu. Serikali ilielekeza halmashauri zote (mkoa, wilaya, miji na vijiji) kutenga asilimia kumi (10%) ya mapato ya ndani kama mikopo nafuu kwa makundi maalumu. Utaratibu wa kutoa mikopo nafuu kwa makundi maalumu ulisitishwa na serikali baada ya kutokea changamoto nyingi lakini kubwa ikiwa ni urejeshaji hafifu wa mikopo iliyotolewa.
Kwa upande mwingine, serikali katika kuwezesha makundi maalumu iliamua kutumia nguvu yake ya kimanunuzi kwa kuelekeza taasisi zote za serikali kutenga asilimia thelathini (30%) ya thamani ya manunuzi yao kwa mwaka kutumika kununua bidhaa, huduma na kazi za ujenzi kutoka kwa makundi maalumu. Utaratibu ukaleta changamoto nyingine katika utekelezaji wake nayo ni ukosefu wa mtaji-pesa (financial capital) ya kuendeshea biashara kwa makundi maalumu. Katika utaratibu wa manunuzi ya umma, miongoni mwa vigezo vingi hupimwa pia kwa uwezo wao wa kifedha wa kuweza kutekeleza masharti ya mikataba ya ununuzi wa umma. Katika muktadha huu ambao makundi maalumu hayana uwezo wa kifedha (inadequate capital access) wa kutekeleza mikataba ya ununuzi wa umma huweza kupelekea kukosa zabuni husika.
Hivyo insha hii inatambua kuwa makundi maalumu yana changamoto ya ajira na umasikini na kwa sasa mipango ya kuwawezesha kiuchumi kupitia mikopo ya halmashauri na manunuzi ya umma yamegubikwa na utata/changamoto ambazo zitafanya makundi maalumu yashindwe kupata faida za kiuchumi na hatimaye kujikwamua kutoka kwenye ukosefu wa ajira na umasikini kwa kutumia mipango husika. Hivyo, natoa pendekezo la serikali kufikiria kufungamanisha mikopo ya halmashauri na ununuzi wa umma kupitia makundi maalumu ili kusaidi kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira. Ufungamanishaji huo wa mikopo ya halmashauri na ununuzi wa umma ufanyike kwa utaratibu ufuatao;
Hatua ya kwanza; taasisi za serikali zitangaze zabuni za ushindani kwa makundi maalumu kama sheria na kanuni zinavyotaka. Kigezo cha msingi cha kutoa mkataba kiwe ni ujuzi na nafuu ya bei inayotolewa na kundi maalumu katika zabuni shindani. Makundi maalumu yasiyo na uwezo wa kifedha yatafanya maombi ya awali ya mkopo kutoka benki (zilizokasimiwa mamlaka ya kutoa mikopo ya 10%). Benki zitatoa barua ya kusudio la kutoa mkopo (letter of intent to fund) ambazo zitaambatanishwa na mkundi maalumu kama uthibitisho kuwa watakuwa na uwezo wa kifedha kutekeleza mkataba wakati wakisubiri malipo ya kimkataba.
Hatua ya pili, taasisi za serikali zitaendelea na mchakato wa zabuni na kundi maalumu litakaloshinda litasainishwa mkataba wa ununuzi. Kundi maalumu lililopatiwa mkataba wa ununuzi watawasilisha nakala ya mkataba benki kama dhamana kisha watapatiwa mkopo hadi kufikia asilimia 60-75 ya thamani ya mkataba (contract financing) ili kuwezesha kundi maalumu kuwa na fedha ya kutekeleza mkataba husika kwa kununua rasilimali zinazohitajika (material, vifaa, posho n.k). Kiasi cha mkopo kitakachotolewa kiendane na muda wa mkataba. Dhumuni la kusema hivi ni kuwa kama mkataba ni wa miezi minne basi deni na riba yake litalipwa mara moja baada ya kundi maalumu kulipwa fedha za kimkataba. Mfano, kama mkataba una thamani ya 50,000,000/- basi kundi maalumu litakopeshwa kiwango cha juu cha 37,500,000/- na kama riba ya rejesho la mkopo ni 3% kwa mwezi maana yake baada ya miezi minne riba itakuwa 12% sawa na 4,500,000/- hivyo kufanya rejesho lote kuwa 42,000,000. Katika hesabu hii kundi maalumu litabaki na faida/nyongeza ya mtaji kiasi cha 8,000,000. Hesabu hii ni mfano tu hivyo hauoneshi kodi zitakazotozwa kutokana na biashara husika. Pendekezo la malipo kufanyika mara moja inatokana na ukweli kwamba makundi maalumu hayategemewi kupata mikataba ya muda mrefu tofauti na wakandarasi/wazabuni wa kawaida.
Hatua zinazofuata zitajumuisha kundi maalumu kutekeleza mkataba na kama utekelezaji ulifanyika kwa kiwango cha kuridhisha basi kundi husika litadai malipo yake ambapo taasisi ya serikali inayotakiwa kumlipa kundi maalumu itawasiliana na benki husika ili kufanikisha rejesho la mkopo kama ambavyo taasisi hizo zinasaidia benki kwenye kuhakikisha marejesho ya mikopo inayochukuliwa na wafanyakazi wake. Utaratibu huu una faida kwa pande mbili, kwanza unawezesha kundi maalumu kupata fedha za kutekeleza mikataba na kwa upande mwingine unasaidia serikali kuweza kudhibiti utoaji wa mikopo na zaidi kuhakikisha mikopo inayotolewa inarejeshwa ili kusaidia makundi mengine au matumizi mengine ya kimaendeleo. Utaratibu huu unaopendekezwa hapa hauzuii kutoa mikopo kwa shughuliz zingine za makundi maalumu ambazo hazihusishi ununuzi wa umma.

Upvote
2