Kufuatia Royal tour, sasa wizara kubomoa nyumba Kilwa ili ziwe za kisasa

Kufuatia Royal tour, sasa wizara kubomoa nyumba Kilwa ili ziwe za kisasa

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
05 May 2022

SIKU YA KUADHIMISHA URITHI WA DUNIA AFRIKA, WIZARA KUBOMOA MAJENGO YA URITHI KILWA


Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia mamlaka ya usimamizi wanyama-pori TAWA ikiadhimisha siku ya urithi wa dunia Afrika imesema ina mpango wa kuboresha mazingira ya Kilwa Kisiwani kwa kubomoa nyumba zenye urithi wa historia, tamaduni ambazo zimenakiliwa katika historia ya eneo hilo.
1651782030032.png


Wizara imesema kuwajengea nyumba mpya za kisasa kutafanya wenyeji kuweza kuwa na nyumba za kisasa kuweza kuwa B& B ya vyumba viwili, chumba cha wageni, jiko na maliwato ili kunufaisha wenyeji wa Kilwa na pia malazi kwa wageni na watalii watakaotembelea eneo hilo lenye urithi wa majengo, utamaduni na mila zinazotambulika kama urithi wa dunia kupitia UNESCO





Hata hivyo wenyeji wa Kilwa wanajivunia historia yao na wanapenda nyumba chakavu za kihistoria kufanyiwa ukarabati na kuongezewa vitu vya kisasa bila kupoteza asili ya nyumba hizo zenye muundo, nakshi, sanaa za asili, nyimbo, tamaduni na muonekano wa kusimulia historia ya karne kadhaa za wenyeji na wageni walioishi hapo kwa mamia ya miaka ambavyo huwezi kuvikuta isipokuwa Kilwa Tanzania.

Kule nchini Ugiriki, Italian n.k maeneo ya urithi wa kihistoria na utamaduni wa karne nyingi huhifadhiwa na kubakishwa kwa muonekano huo wa kale huku mazingira yake yakiboreshwa bila kuathiri urithi unaovutia watalii na wenyeji pia wanaopenda kutembelea eneo linaloweza kufananishwa na makumbusho ya wazi ( Open Museum).

Msanii wetu mtanzania alitumia fursa kama hiyo ya mandhari ya kipekee ya historia ya Ugiriki na kutengeneza wimbo wake ambao pia kiaina umefanikiwa kutangaza mandhari zilizotunzwa kwa mamia ya miaka na kuwa sehemu inayovutia watalii kwa mamia kutembelea Greece kutokana na upekee wa eneo hilo linalobebwa kihistoria na kitalii .




MAONO YA MH. RAIS, ZIARA YAKE KUITANGAZA KUPITIA TANZANIA ROYAL TOUR

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezindua filamu ya Tanzania iliyopewa jina "The Royal Tour" nchini Marekani. Serikali imesema filamu hiyo itaitangaza Tanzania duniani. Je, itakuwa na ushawishi gani katika sekta ya utalii Tanzania bara na visiwani Zanzibar?​

 
MJI MKONGWE WA STONE TOWN ZANZIBAR UMEKUWA KIVUTIO KWA MAMIA YA WATALII

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kushirikiana na UNESCO pamoja na wadau wengine wanauenzi na kulinda urithi wa eneo hilo lenye upekee duniani

 
Toka maktaba

06 JANUARY 2022

Dc Kawawa Awaita Wawekezaji Kilwa Kisiwani, Songo Mnara​


Wananchi wilayani Kilwa mkoani Lindi, wametakiwa kuchangamkia fursa za uwekezaji katika sekta ya utalii kufuatia uamuzi wa dhati uliyochukuliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), kufungua milango kwa kutangaza vivutio vinavyopatikana katika wilaya hiyo.

Wito huo umetolewa hivi karibuni na Mkuu wa wilaya hiyo Bi. Zainabu Kawawa, ambapo amesema TAWA inafanya kazi kubwa ya kutangaza utalii wa kusini hususan unaopatikana katika wilaya ya Kilwa.

Ameongeza kuwa pamoja na kazi kubwa inayofanywa na TAWA ya kutangaza vivutio vya utalii vinavyowavutia watalii kutoka ndani na nje ya nchi. mamlaka hiyo imeweka mazingira rafiki kwa watalii kwa kununua boti ya kisasa.

Mkuu huyo wa wilaya amesema, boti hiyo ina uwezo wa kusafirisha watalii kutoka kisiwa kimoja hadi kingine, huku wakifurahia kuangalia viumbe mbalimbali wa majini wakiwa ndani ya boti hiyo.

Amesema utalii wa majini unaopatikana katika visiwa vya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara, ni pamoja na utalii wa Matumbawe, ambao watalii wanaweza kuona viumbe vya chini ya bahari kupitia boti ya kisasa iliyonunuliwa na TAWA.

Vivutio vingine ni utajiri mkubwa wa historia kupitia malikale (magofu), ambao kwa upekee wake, umeingizwa katika orodha ya urithi wa dunia, inayotambuliwa kimataifa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

"Mbali na magofu yanayopatikana, pia mtalii anapopata fursa ya kutembelea visiwa hivyo atapata muda wa kufahamu historia nzima ya mji wa Kilwa na uzuri wake, tangu karne ya 13 pamoja na kufurahia upepo wa Pwani kutoka bahari ya Hindi," amesema.

Kwa upande wake Samson Gisiri, Mhifadhi kutoka TAWA, ambao wamepewa dhamana ya kusimamia malikale, alisema moja kati ya kazi ya mamlaka hiyo ni kusimamia na kutunza malikale zilizopo katika visiwa vya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara.

Aidha, ameongeza kuwa katika kuweka mazingira rafiki kwa watalii, TAWA imeanza kujenga sehemu maalumu za malazi kwa ajili ya watalii Kilwa Kisiwani, ili kuwafanya wafurahie muda wao katika visiwa hivyo.

Mhifadhi huyo amewataka Watanzania kutembelea maeneo ya Songo Mnara na Kilwa Kisiwani, ili kujionea urithi wa dunia unaopatikana katika visiwa hivyo.

Source : MUUNGWANA BLOG
 
Wasisahau kubomoa na yale masanamu yanaonesha watumwa kule bagamoyo,Yan me ningekua rais ningeshabomoa siku nying na story za utumwa zisingefundishwa mashuleni haya mambo ndio yanafanya waAfrica wawe wanyonge kwa hawa wazungu na waarab!na wao kutuzarau jamaa wanaleta watoto kuja kuona mambo ya mababu zao walivyofanya sad!
 
Walafi wamepatamani hapo, sipafamu lakini kwa hii Serikali ilivyo, tayari hilo eneo ameshapatiwa mtu.
 
Wasisahau kubomoa na yale masanamu yanaonesha watumwa kule bagamoyo,Yan me ningekua rais ningeshabomoa siku nying na story za utumwa zisingefundishwa mashuleni haya mambo ndio yanafanya waAfrica wawe wanyonge kwa hawa wazungu na waarab!na wao kutuzarau jamaa wanaleta watoto kuja kuona mambo ya mababu zao walivyofanya sad!
kumbukumbu zibaki ili na watoto wetu wajue madhila waliyopitia babu zao, ili tujifunze kujitegema na kupunguza kujikomba kwa watu ambao hawana nia njema nasi bali maslahi yao binafsi
 
Back
Top Bottom