Kufuatia video inayohusu tukio la utekaji Mohammed Kawaida asema ni movie kama movie zingine zenye lengo la kupata huruma kwa wananchi

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mwenyekiti wa UVCCM Mohammed Kawaida kupitia mtandao wa Instagram akijibu post ya Twaha Mwaipaya ambaye alichapisha video iliyorekodiwa katika eneo la Kiluvya Madukani jijini Dar es salaam ambapo inaonesha tukio la utekaji ambalo halikufanikiwa, Kawaida amesema

"Hii ni movie kama movie nyengine tuuu munazoendelea kutengeneza kwa lengo la kupata huruma kutoka kwa wananchi, ndugu yangu @twahamwaipaya tukutane serikali za mtaa. Watanzania wanahitaji maendeleo na sio maigizo ya kutengeneza"

Pia soma: MAKALA: Ni kujidanganya kama Taifa kusema mauaji na utekaji ni mambo ya kawaida

 
Huyu dogo anaonyesha katili sana,Baba wa watu alivyokuwa akilia na kuomba msaada vile!
 
Kwa Uandishi huo huyu Bw mdogo atakuwa Mzanzibar. Ni ishara tosha hawa watu hawana utu wala huruma kwa Watanganyika tuchukue tahadhari kubwa hawa viumbe watatuua watumalize, hawana utu wala tone la huruma mioyoni mwao.
lakini wamejulikana waliotaka kuteka
 
Kwa Uandishi huo huyu Bw mdogo atakuwa Mzanzibar. Ni ishara tosha hawa watu hawana utu wala huruma kwa Watanganyika tuchukue tahadhari kubwa hawa viumbe watatuua watumalize, hawana utu wala tone la huruma mioyoni mwao.
Wazanzibari huwa wanajijali wao ni wabinafsi.
 
UVCCM kwa sasa imejaa watoto wa vigogo wasio na utu kabisa. Huyo kawaida ni mtu katili. Hawa vijana hawakisaidii chama zaidi ya kukiharibia zaidi. Kule Arusha mwenyekiti wa UVCCM ni mtoto wa Meya. Hawa vijana wakiendekezwa watachochea CCM kuondolewa madarakani.
 
Kawaida ni aina vijana wa KAWAIDA waliojaa chama cha interahamwe
 
Na ile ya Iringa ya mtu kutwangwa shaba anasemaje?
 
Imagine, huyu nae ni kiongozi, haishangazi kuiona Tanzania 🇹🇿 hii ya leo baada ya. Iaka 60+ wamama vijijini wanasaka maji kilometa 5 mpaka 10.

Jana nimesoma sehemu umasaini huko, wakiwa kipindi cha hedhi wanatumia mpaka mikojo ya ng'ombe kujisafisha, maji ni changamoto kubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…