Kufugiwa kwa niaba na kulimiwa kwa niaba

Kufugiwa kwa niaba na kulimiwa kwa niaba

MURUSI

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2013
Posts
4,537
Reaction score
8,824
Hii nchi wajinga ni wengi mno na hawataisha, yaani mtu hawezi hata ku-reason. Kweli kama kilimo kinalipa kuna mtu kweli atanyanyua mdomo kusema njooni tuwalimie kwa niaba yenu?

Au kama ufugaji wa kuku unalipa kuna atakayehangaika na watu au atataka sokoni awe peke yake na apige pesa?

Sijawahi sikia Bakhresa anasema juice zinalipa sana na Watanzania wanaotaka kuwekeza wamuone.

Hii nchi ina watu wavivu na wajinga kupindukia, na hawataisha milele hadi siku ya kiama.
 
Mr.Kuku ndio alitumiaga fursa. Ujinga mwingine ni Network marketing, yaani majitu majinga yale sijawahi ona, eti lete milion 5 tukupe cheni, halafu kila mwezi unaingizwa dollar 200 maisha yako yote , stupid!!!!
Week Iliyopita Nimemsikia Mr Kuku Kwenye Kituo Kimoja Cha Radio
Anawatangazia Umma Anauza Kuku Wa Nyama. Na Vipande, Vichwa, Mabawa, Mapaja
Moyoni Nikasema Tariq Machibya Karudi
Atawapiga Haraka Sana
 
Huo ni mfumo wa shea.....
sema upo kizamani/kijima....
hakuna jipya hapo ni kama kampuni zilizokuwa registered public...
zinapouza shea......
na ww unakuwa sehemu ya umiliki kwa saizi ya shea ulizonunua
 
Penda kufanya tafiti ndugu....huo ni uwekezaji kama uwekezaji wa hisa tu..mwingine ana muda na utaalamu na soko kubwa lakini hana pesa ya mtaji kukidhi soko hilo...mwingine ana pesa ya mtaji wa kufanya investiment lakini hana muda so anampa pesa mwenye Muda,utaalamu na soko ili azalishe then wanagawana faida...

Mtu akiingiza utapeli humo ni utapeli tu kama utapeli mwingine lakini hivyo vitu vipo real cha msingi kuwa makini tu.
 
Uko sahihi. Hata Mimi nimekuwa nawaza hii fursa kitambo Sana. Kwa sababu napenda ufugaji tangu utotoni Ila kwa Sasa Sina muda Wala eneo la kutosha
 
Biashara ya ufugaji kuku!!!! Tusikumbushane wakuu ,ushauri wangu kama ww ni mpenda kula kuku usifuge kuku, maana utazila mwenyewe ushuhuda ni mm hapa.
 
Ukitaka kulima lima mwenyewe aisee na uwe unaenda shamba daily. Kuna mpumbavu mmoja alinishauri tulime mihogo nilichokikuta ni mavimavi tu .Kwanza matuta yapo kama S mengine kama Z. Nyasi kibao mihogo haionekani.Lilivyo jinga linaniambia mihogo haifi we subiri tu mvua irudi mwezi wa 11.Kwa hasira nimelizira shamba atajua mwenyewe
 
Ukitaka kulima lima mwenyewe aisee na uwe unaenda shamba daily .Kuna mpumbavu mmoja alinishauri tulime mihogo nilichokikuta ni mavimavi tu .Kwanza matuta yapo kama S mengine kama Z.Nyasi kibao mihogo haionekani.Lilivyo jinga linaniambia mihogo haifi we subiri tu mvua irudi mwezi wa 11.Kwa hasira nimelizira shamba atajua mwenyewe

Pasua kichwa hao ww acha tu. Mm naenda nao bega kwa bega mpk wamenitunga jina MKUDA. Cku za shamba tulizo kubaliana zote nipo nao. Ukifanya ivyo matokeo unapata grade A
 
Pasua kichwa hao ww acha tu. Mm naenda nao bega kwa bega mpk wamenitunga jina MKUDA. Cku za shamba tulizo kubaliana zote nipo nao. Ukifanya ivyo matokeo unapata grade A
Nakubali mkuu usiwape gap kabisa hao
 
Dah huu uzi umenigusa kidogo.
Hipo hv wakuu, ukiMua kulima u should be there always. Yaan Shamba linahitaji usimamizi wa hali ya juu, ukisuasua tu unaharibu Kila kitu. Ni ngumu sana kulima huku unakumbatia Ajira thus why watu huwa wanaingia ubia with fellow yaan
 
Back
Top Bottom