Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mapema mwezi Juni Yanga walifanya Mkutano Mkuu na hapo ndipo walimtangaza Miguel Ángel Gamondi kuwa ameongeza mkataba wa mwaka mmoja na kutokana na mafanikio yake na Wananchi ya msimu wa 2023/24 basi walikuja na msemo wa "TABU IKO PALE PALE" kutokana kuwatesa sana Watani zao Simba SC.
Soma, Pia: Rasmi: Yanga yavunja Mkataba na Gamondi
Kama surprise mbele ya Wanachama wa Yanga Gamondi alidai ametokea Club kwenye show ya Marioo baada ya kuulizwa na Rais wa Yanga, Eng. Hersi na ukumbi mzima ukaripuka kwa furaha bila kufikiria kuwa wanatengeneza tatizo.
Kwenye moja ya sababu za kutimuliwa Master Gamondi inadaiwa kuwa ni ishu ya kinidhamu ambayo ilipelekea kuwa na kundi la wachezaji ambao inaelezwa alikuwa anatoka nao kwenda kula bata.
Tatizo la kinidhamu waliendekeza wenyewe viongozi ila limeondoka na kibarua chake
Miguel Ángel Gamondi aliteuliwa kuwa kocha mkuu wa Yanga, akichukua nafasi ya Nasreddine Nabi. Aliongoza Yanga kushinda taji la Ligi Kuu ya Tanzania kwa mara ya 30 na kufikia robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Soma: Kocha Kheireddine Madoui wa CS Constantine kuchukua Mikoba ya Gamondi Jangwani