Kufukuzwa kwa Halima Mdee na Wenzake 18 na mkanganyiko wa Ubunge wao

Kama tume imechafuliwa ungewashauri waende mahakamani.....
 
Chadema ni watu wabaya sana kwenye medani ya siasa wanendekeza mapenzi kuliko uhalisia mnyika alipeleka majina na nyaraka zote husika tume zikapokelewa na zikapekekwa kwa spika ndiyo wakaapishwa ndiyo maana chadema huwaga hawajibu swali hili kwanini wasiende mahakamani kama majina na nyaraka za uteuzi zilifojiwa? Je hiyo siyo jinai? Hapo wanapata kigugumizi maana hakuna fojari hapo document halali wanachofanya ni ubabe kisa demu wa mbowe hakuwemo kwenye orodha kakosa ubunge
 
Mkuu;
Ukisoma kifungu cha 86A cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343. Utaelewa namna Viti maalum vinapatikana.
Documents ikishasainiwa na responsible person ikawa na ithibati zote za chama kwa mujibu wa sheria hiyo huwa ni document halali. Haijalishi nani anapeleka. Nikupe mfano, "pendekezo la jina la Waziri Mkuu hutolewa na Rais, lakini halipelekwi na Rais Bungeni"
Muhusika ndani ya chama akimaliza taratibu za ndani ya chama anaweza kumtuma secretary au yeyote anayeona anafaa aiwasilishe hiyo document sehemu anayotarajia kuifikisha.
Ikumbukwe; orosha ilihitajika 30 days before general election [emoji2][emoji2]
 
Sasa kama hujui kitu si ungeuliza kiliko kujiita Single Burtan kumbe hata batan yenyewe huna.
1.Kabla ya uchaguzi Chama kinapeleka majina.
2.Majina yanahifadhiwa na Tume Kwa sifa zilizoainishwa ikiwa ni pamoja na kujua kusoma na uhalali wa uanachama.
3.Uchaguzi Mkuu unaendeshwa na Kura zinapigwa.
4.Tume inapiga hesabu Kila Chama kinastahili kupata Viti maalum wangapi kutokana na Kura za Urais na idadi ya Wabunge majimboni.
5.Tume inakiandikia Chama husika kukijulisha idadi ya Viti maalum kiliopatiwa.
6.Chama kinapeleka majina kulingana na idadi kilichoandikwa na Tume kutokana na majina yaliyoko Tume. Ni kama mahakamani mlalamikaji anavyotaja mashahidi wake na si lazima wote watoe ushahidi Ila haruhusiwi kuleta mashahidi wapya.
7.Baada ya Tume kupokea inaangalia kama waliopelekwa bado Wana sifa.
8.Inateua na kumpelekea Spika orodha ya Viti maalum vya Chama husika.
NB; Hii ndo maana ya Tume kujadiliana na Chama husika kuhusu uteuzi wa Viti maalum.

Vinginevyo tume ingechukua orodha na kuandika majina inayoona yenyewe toka kwenye orodha na kuyapeleka Bungeni.
Kwa hiyo Acha kupotosha Kwa usichokijua.

Sent from my M2003J15SC using JamiiForums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23] daaaah, haya bhana.
 
Kwani hawa watu, siwalishafukuzwa siku nyingi tu, ipi tofauti ya awali na sasaivi kufukuzwa kwao
 
Nakushauri Kasome maelekezo ya ibara ya 86A sura ya 343 ya sheria ya Taifa ya Uchaguzi na uielewe, itakusaidia kujikosoa kwenye upotoshaji ulio katika hili andiko lako lakini pia utaelewa vizuri mantiki iliyopo katika andiko langu.
 
Mwanzo walifukuzwa bila kufuata taratibu
Na sasa wamefukuzwa "tena" mara nyingine kwa utaratibu wa kidemokrasia[emoji2][emoji2]
 
Huna cha mantiki labda matiki.

Upo sahihi kabisa ndugu.na ndio maana hata mbunge wa viti maalum anapofariki tume hurudi kwenye orodha na kuchukua jina linalofuata,katika hili mahakamani ni suluhisho la yote.
 
1. Kama hao wabunge 19 wa Chadema walighushi saini ya katibu mkuu wa chama, kughushi mhuri wa chama na kuandaa na kupeleka orodha ya majina bungeni na ushahidi usio kuwa na shaka upo bayana basi wawasiliane na DPP wafunguliwe kesi maana ni makosa ya jinai sio nidhamu pekee
2. Kama kwa kujua bunge lilipokea majina kutoka kwa mwakilishi yeyote wa Chadema kinyume na utaratibu na kuhalalisha ubatili basi katibu wa bunge, spika, naibu spika na kamati husika ambayo kwa vyovyote vile ni sharti majina hayo yaitie kwao kabla ya kutangazwa hadharani na mhimili huo basi wanapaswa kuwajibishwa kwa spika na naibu wake kuondolewa kwenye nafasi za uongozi na wale wengine kama katibu wa bunge ambaye ndiye mtendaji mkuu na mwakilishi wa serikali pamaja na kamati husika wanapaswa kufunguliwa mashitaka maana wametenda makosa ya jinai
3. Kama kuna ushahidi kwamba majina ya wabunge wa viti maalum pendekezwa ni sharti yapelekwe na katibu mkuu lakini kwa mazingira ya kesi husika aliyepeleka hana mamlaka ya chama chake basi alipokea hati hizo anatakiwa kushitakiwa pia kwa kuvunja sheria kwa makusudi kwa maslahi binafsi
4. Je, kanuni za bunge zimevunjwa kutokana na maamuzi ya chama cha Chadema kuwafukuzwa wanachama wao? Maana kila kosa linapotendwa huwa kuna muda maalumu wa kuwasilisha lalamiko husika?
5. Kama chama cha Chadema kiliwakataa wabunge 19 waliokuwa wakiwakilisha CDM kwa sababu mbili za kutotambua uteuzi wao na matokeo ya mwaka 2020, je kuwaengua hao watapendekeza wengine waende bungeni kwa uhalali upi unaotokana na kura iliyopigwa wakaikubali?
6. Takribani mwaka mzima sasa wale wabunge wanahudhuria bungeni na kwa mjibu wa sheria chama kinachowakilishwa kinasitahili kupata ruzuku kwa uzingatia asilimia ya uwakilishi, je, Chadema watakuwa na uhalali upi wakipeleka tena wabunge kisha wakakubali kupokea ruzuku waliyoisusia tangu uchaguzi ufanyike mwaka 2020 hadi sasa?
7. Endapo Chadema watadai limbikizo la ruzuku tangu mwaka 2020 hadi sasa itakuwa ni wizi na wanastahili na wenyewe kushitakiwa au kufutwa
8. Kama kuna viongozi wa CCM waliwasimika hao wabunge ndani ya bunge kwa maslahi binafsi, wanatakiwa kushtakiwa kwa mjibu wa sheria
 
Mwanzo walifukuzwa bila kufuata taratibu
Na sasa wamefukuzwa "tena" mara nyingine kwa utaratibu wa kidemokrasia[emoji2][emoji2]
Walifukuzwa na kamati kuu, wakakata rufaa halmashauri kuu. Halmashauri imeridhia uamuzi wa kamati kuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…