Kufukuzwa makocha hawa ni kielelezo cha kiwango kidogo cha ufahamu Tanzania

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Kwanza kafukuzwa Zahera,mara Upande wa pili nao wamemfukuza Patric mwalimu aliyeipeleka simba ktk hatua ya fainali za klabu bingwa afrika katika historia baada ya miaka mingi..leo ati anaambiwa hafai aondoke!

Hivi tatizo ni walimu kweli?Juzi hapa tumeshuhudia Yanga ikihangaika kutafuta kuishinda timu ndogo na mpya kwenye ligi Kmc na kuishia suluhu..!

Hivi mnaonaje viwango vya wachezaji wetu wazawa hapa tz?

Hadi Leo Ngasa,Kaseja wanaanza first eleven!

Sie wengine tumejikita ktk kufuatilia na kushabikia soka la ulaya miaka mingi..kwa kweli si kwa ubaya lakini niseme huwa nashangaa sana watu wanaoshabikia soka la tz..siwaelewi kabisa.

Watu watafakari hivi hizi timu zitakuja kaana makocha wazuri kweli?

Simba unamuondoa Patric kweli? Marcio Maximo??!..pole Tanzania.
 
Umewaza kipumbavu sana. Makocha hata ulaya wanafukuzwa labda uwe hufuatilii tu ligi za wenzetu. Kocha kama anataka kuwa juu ya team anafukuzwa.kocha kama hafikii malengo ya team anafukuzwa.

Kocha simba amekaa mwaka mmoja kuna mambo kapishana na viongozi. Anaondoka.kama unampenda sana si umchukue akae nyumbani kwako.

Kabla ya kocha huyo alikuwepo mwingine na mwingine na mwingine na mwingine. Wanakuja wanaondoka.team inabaki.hata ulaya wanafukuza acheni upumbavu.mnapenda jifichia sana ulaya ,ulaya kunani huko ulaya? Kama yanga hawakurishika na Zahera ulitaka wakae naye tu kwani Mkeo wao?

Kocha kama hayupo sahihi atafukuzwa tu. Wala haina kuremba hiyo. Na mimi nasema kama kocha akiambiwa fanya hivi halafu hasikii akajiona yeye ni mkuu afukuzwe tu.
 
Punguzeni uswahili, haya mambo ndo yanazcost timu kubwa Ulaya hasa Chelsea na Man u, mwenye jukumu zito kwenye timu ni Kocha , viongozi wanahtaj matokeo, lakn matokeo Yana mikakati yake , ni vyema kocha akasikilizwa , sio kumtupia vilago tu, kocha anajitahd kufanya sehemu yake Ila viongozi hawafany sehemu Yao, kocha analeta mapendekezo nyie mnayapiga teke na bado mnahitaji matokeo , alaf mnaleta bla bla et hasikilizi viongoz , punguzeni ushehe kwenye proffessional za watu...

Mmezoea kupanga matokeo nje ya uwanja hamuhtaj kugharamika....

Guardiola mwaka wa Kwanza mancity walikula hasara vibaya ovyo , chupu chupu akose hata top4, Liverpool vile vile, lakn kocha alisikilizwa akatimiziwa mahtaj yake kwa , kocha anapoleta mikakati yake ni vyema akasikilizwa ili akishindwa basi abebeshwe zgo la lawama anapostahili, sio mmekalisha matumbo yenu tuu mnawaza biashara bila kuwajibika , alaf mnakuja na mawazo mfu, et kocha hasikilizi viongozi....
 
Huu uswahili upo hata ulaya? Tena kwa Clubs Kubwa?
Kocha anapoajiliwa anapewa mkataba ambo kuna mambo watu wanaandikishana ai lazima wayaweke wazi.mmoja wapo anapovunja hayo makubaliano mkataba unavunjwa.

Patrick alipewa nafasi ya kusikilizwa hakutoa majibu mujarabu ulitaka wambembeleze? Sidhani. Simba wana akili na wanajua nini wanafanya kuliko sisi huku wapiga kelele.kama Mo Dewj kaweka Billions zake wewe ina maana una uchungu kuliko yeye? Hapa si nikutumia tu akili nyepes za kawaida
?
 
blah blah blah
 
Baada ya manji kuwapiga chini? Nyie si mlienda kuosha gari yke pale centre?kipindi kile anataka kuwakodi?πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Sasa mnalo wananchi n shida zenu.simba acha ienjoy tu mi nashauri Mo Dewj ainunue kabisa iwe yake. Wanasimba wanachofurahia ni kuwa wachezaji wanalipwa mishahara na viwanja vinaonekana vikikamilika huko Bunju. Baada ya kumkosa manji sasa mnawaya waya tu.na zahera mlipeni pesa zakem

Club ya Wananchi ipo moja tu - Yanga.
Simba ni bidhaa ya Mo Dewji.
 
Simba chini ya Aussems tayari ilishapoteza points 5 ligi ikiwa mbichi kabisa, more so, unafungwa na Mwadui kwa kupanga kikosi ambacho kila mtu alijua kabla ya mchezo kuwa kitafungwa kutokana na nature ya uwanja.

Hivi yeye hajui kuwa kwenye viwanja vibovu anatakiwa kuwapanga wabongo ambao wamevizoea, mbona alifanya hivyo na biashara tukapata matokeo kwanini asingefanya the same kwa Mwadui, anaonekana hana track record ya michezo yake.
 
Sawa wacha tungoje tuone watakaokuja ninaamini Tz hata aje Pep mtamfukuza tu eti kisa timu haipeform vizuri...yajayo yanafurahisha
 
Unadhani pep watamwogopa sababu ya jina?chelsea walimfukuza jose m sababu haikufanya vizuri, man chest wakamtimua pia.ukiangalia mpira majina utapotea kama team haiperform vizur mi nashauri coach afukuzwe tu hamna kuremba. Watu wanataka matokeo kama majina hata mbwa wanayo.

Sawa wacha tungoje tuone watakaokuja ninaamini Tz hata aje Pep mtamfukuza tu eti kisa timu haipeform vizuri...yajayo yanafurahisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…