Kufunga chakula inaweza kuwa mwanzo mzuri wa kubadili mwenendo wako mbaya

Kufunga chakula inaweza kuwa mwanzo mzuri wa kubadili mwenendo wako mbaya

musicarlito

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2020
Posts
368
Reaction score
556
Wasalaam

Wakuu mwezi huu ni wa heri kweli

Madhehebu makuu mawili kwa asilimia kubwa wako katika mfungo,japo kila moja lina namna yake na makusudi yake,lakini lau wote wanalenga kuwa na mahusiano mazuri na Mungu.

Mungu ni mwanga...tunavyozidi kumkaribia au kuonesha juhudi za kumkaribia,anatumulika na kutusahihisha katika yale yanayopunguza thamani na heshima ya utu wetu mfano ulevi...ukahaba...wizi na majina yote mabaya.

Kufunga ni njia nzuri ya kujidhiri...tunapojidhiri/kujishusha...tunamwachia Mungu nafasi katika maisha yake aoneshe nguvu zake

Namna ambazo zimekuwa ngumu kuzishinda kama ulevi na tabia zozote mbaya,kufunga inaweza kuwa mwanzo mpya wa matumaini...wakristo mnafahamu hapa Mt 17:21
Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga

Kumbe wale mnaotamani kweli kuwa watakatifu mkiamini kuwa hatukamiliki kamwe ila tunakamilishwa na Mungu mwenyewe,tuijaribu njia hii

Samahani msioamini kuwa kuna Mungu au msiomwamini hata kama yupo,sijawalenga katika bandiko hili
 
Back
Top Bottom