Kufunga chakula katika imani ya kikristo ni suala la kujitangaza au ni siri binafsi?

Kufunga chakula katika imani ya kikristo ni suala la kujitangaza au ni siri binafsi?

raslimali

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
1,958
Reaction score
1,744
Yesu alisema ukifunga jiweke uso wako vizuri kwa mafuta ili mtu asijue unafunga. Ni dhahiri kwa mafundisho yake funga ya mkristo ni suala binafsi na ni siri ya anayefunga.

Vipi leo haya maredio ya makanisa yanatangaza mifungo kila uchwao mara mfungo wa siku ishirini na moja wa mwaka wa utawala, mara mfungo wa siku nzima, mara mfungo wa siku arobaini? Mafundisho ya wapi haya?
 
Mafungo ni siri, ila kuna mafungo ya makundi au watu wengi wengi, hapo sometimes inakuwa wazi.

Mungu anaangalia Moyo.

1 Sam 16:7 SUV

.. .... maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo.
 
Wapo sahihi mkuu hio mifungo ya jumuia kwaajili ya jambo flan na baada ya hapo ni siri ya kila aliefunga na Mungu wake, lets kwa mfano sisi kama taifa tumeamua kufunga kuombea nchi ni lazima tutangaziwe tarehe ya kuanza kumaliza
 
Mtu binafsi anapofunga na kutangazia watu na kila saa kujisemesha semesha oh swaumu kali, oh ngoja nikafuturu hilo ni kosa kubwa ktk ukristo. Kukaa unatia tia huruma unataka kila mtu awe attention na kufunga kwako hilo ni kosa. Ila mifungo ya watu wengi lazima itangazwe, rejea story ya Esta ktk bible, pia Ezra na wengineo.
 
Back
Top Bottom