Kufunga mtungi wa gesi ORYX

Mtu Poa 2013

Senior Member
Joined
Mar 26, 2013
Posts
105
Reaction score
65
Habari. Kutokana na High pressure regulators za mitungi ya gesi kuwa ghali sana kwa sasa, je inawezekana badala ya kuweka high pressure regulator nikafunga na mpira?
 
Habari. Kutokana na High pressure regulators za mitungi ya gesi kuwa ghali sana kwa sasa, je inawezekana badala ya kuweka high pressure regulator nikafunga na mpira?

Ghali shilingi ngapi mkuu,may be nilinunua zaman sana lakin angalia madhara ya kufunga na manati na kuingia gharama,mie nakushauri jipange tu ununue
 
Habari. Kutokana na High pressure regulators za mitungi ya gesi kuwa ghali sana kwa sasa, je inawezekana badala ya kuweka high pressure regulator nikafunga na mpira?

Mkuu mimi sijakuelewa vyema. Ni kwamba hutaki kutumia regulator? Utafunga vipi na mpira? Au regulatore yako haifungi vyema hadi utumie mpira? Pia kutumia high pressure regulator inategemea na kazi husika. Regulator inacontrol kiasi cha gas kutoka kwenye mtungi.
 

Kuna jamaa aliniambia zinauzwa bei ghali. Semma niliamua kuzungukia mwenyewe maduka ya gesi oryx wanauza 90000 ila mihan ni 70000, so ntajipanga nikanunue ya mihan.

Wanaofunga kwa mpira kumbe ni kwamba, kuna watu wanachongesha high pressure regulator na kuziuza kwa 20,000 ila unapoifunga kwenye mtungi inabidi uisupport kwa kufunga na manati kwa juu. Siku hizi kila kitu kinafojika.
 
Watanzania tunatakiwa kujifunza, hivi vitu rahisi mara nyingi huwa vinatugharimu uhai wetu. Nunua regulator original siyo hiyo ya kuchonga kienyeji, itakuletea matatizo tu.
 

Mkuu chunga sana unaweza sababisha majanga makubwa sana endapo ikitokea uvujaji wa gas. Gas ya BUTANE inatabia ya kufuata moto ukiwa karibu kwa vile ni nyepesi sana kuliko hewa. Unakwepa 90,000 lakini utajikuta unapata hasara ya 90M. Nakushauri ni vyema kutumia automatic regulator ambayo hairuhusu gas kupita kama kuna uvujaji wa gas kwenye pipe. Kwa vile umezoea njia za mkato, usije ukajaribu kulazimisha kutumia mtungi ambao hauna rubber ndani ya valve. Kwa sababu gas itaendelea kuvuja na moto ukiwa karibu mtungi utakulipukia na ghafla utasahau majina yako! Unajua kama butane ikivuja itachangayikana na hewa iliotuzunguka (oxygen) na moto ambao hajatarajiwa ukiwa karibu lazima majanga yatatokea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…