Kufunga shule

chetuntu

R I P
Joined
Jan 10, 2011
Posts
949
Reaction score
111
Wadau mnakumbuka kupigana siku ya kufunga shule enzi za mwalimu, ukigombana na mwenzio unamsubiri siku ya kufunga shule. Tukumbusha ulishawah kubondana siku kama hiyo.
 
hakyananani usinikumbushe mablia wakati niko vidudu( chekechea) kuna kijamaa kilinivizia na kunipiga ngwala na kukimbia to make things even worse kwao walihama so tulipofungua sikukaona... hakyanani nakatafuta mpaka leo ukimuona mwambie NIKIMKAMATA lazima nimrudishie ngwala kama ule alionipiga kimagendo.... alooo sisahau mpaka leo
 
Ukimwangusha mwenzako chini basi wewe ni mshindi.
Ukitokwa na damu puani au mdomoni utatafuta upenyo wa kukimbia
 
Dah umenikumbusha mbali sana. Mie ndo nilikuwaga mgomvi namba moja wakishindwa kupigana lazima wanitafute nikifika tu wote wanashangilia ila kilichonitokea wakati niko darasa la 2 sitasahau nilimpiga msichana mmoja mpaka leo kuna kiungo hana yaani leo ugomvi sitaki tena hata unichokoze nakuangalia tu
 
Unachora msitari na akiuvuka tu unae!!
 
vishadida vinachukua mchanga upute.. ukiputa unaambiwa ulipe ng'ombe hapo hata kama jamaa umuwezi bac unabidi ujitutumue... kumbuka sheria (sio rasmi) ilikuwa ukitolewa nundu au damu umeshindwa... mashuhuda wataingilia ugomvi huku wakishangilia "katolewa nundu" hapo ukitaka kuendelea na ugomvi unaonekana mkorofi... duh!
 
Me nilikuwa navizia hatua ya kulipa ng'ombe nakupa za uso halafu nakimbia......naacha gumzo la nani ni mshindi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…