Kufunga tairi size 14/70/165/mbele wakati nyuma nina tairi size 14/70/185

Kufunga tairi size 14/70/165/mbele wakati nyuma nina tairi size 14/70/185

msimamia kucha

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2013
Posts
683
Reaction score
551
Wakuu habari za kazi, natumai wengi wenu weekend imeisha poa, naombai maoni yenu nina Gari yangu yangu ni Spacio new model natumia Tairi size 14/70/185 sasa uchumi umeyumba kidogo nataka Tairi za upande wa mbele nibadili kwa maana zimechanika kabisa sasa nataka niweke size 14/70/165 Tairi ni mpya kabisa je haitosumbua ufanisi wa gari kwa maana zile za nyuma bado zitakuwa size ileile 14/70/185 bado ziko sawa naombeni ushauri. Jioni njema.
 
Mimi sio mtaalamu sana, ila tairi size 185/70R14 ni kubwa na pana kuliko 165/70R14. Kibongobongo unaweza kufunga ila ujue gari itanyanyuka nyuma na kudidimia mbele kwa asilimia fulani.
 
Mimi sio mtaalamu sana, ila tairi size 185/70R14 ni kubwa na pana kuliko 165/70R14. Kibongobongo unaweza kufunga ila ujue gari itanyanyuka nyuma na kudidimia mbele kwa asilimia fulani.
185 na 165 ni upana wa tairi.
Yaani sehemu inayokanyaga ardhi.
Haitakuwa na madhara kwa mwinuko.
Kimo cha tairi zote ni kile kile - 70.
Hiyo 14 ni kipenyo cha rim/tairi ndani kwa ndani.
Mimi nimewahi kuchanganya kwa nyuma. Upande mmoja niliweka 175 na upande mwingine 185.
La muhimu/la lazima uweke kiwango cha upepo kinachoshauriwa.
Magari mengi ya van yanatumia 165.
Sifahamu sababu ya kitaalam.
 
Back
Top Bottom