KERO Kufungia line za simu/ kublock sms yenye namba ya simu ndani yake au sms yenye kiwango cha fedha ndani yake

KERO Kufungia line za simu/ kublock sms yenye namba ya simu ndani yake au sms yenye kiwango cha fedha ndani yake

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Los santos

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2021
Posts
1,167
Reaction score
2,591
Aisee nakereka sana na upuuzi wao wa kufungia line yani miezi mitatu tu unakuta line yako kapewa mtu mwingine

Yani kwenye dunia hii ya leo yenye maendeleo kadha wa kadha ambapo mtu anaweza kwenda kenya, Uganda, sudan,America, Europe au hata south africa akakaa miezi kadhaa kama 5 anarudi anakuta line yake imefungwa

Hivi hawa wahusika hawawezi kuweka kwamba line ikikaa miaka 2 au 1 basi waigawe namba ...yani nakereka sana na huu upuuzi wao wa kufungia mapema

Kingine kuna mtindo unamtumia mtu sms yenye mambo kuhusu fedha au namba ya kukutumia hela unakuta haifiki wanaiblock kisa tu kuinasibisha na zile sms za matapeli yani sjui wataalamu wetu akili zao wanaziweka wapi au zimeishia wapi

Kiukweli wataalamu kwenye mitandao ya simu inabidi wajitafakari sana kama wameshindwa kuzuia wezi basi wasisumbue wengine tukiwa tunashughulika na huduma zetu.
 
Back
Top Bottom