Kufungia redio za dini ni kutatua tatizo au kuficha tatizo?

gogo la shamba

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2013
Posts
6,669
Reaction score
2,165
Wana JF nimetoa hoja hii kwa kuwa naamini kwamba kwenye huu mtandao watu wanatoa mawazo yao kwa uhuru zaidi na kwa uwazi, mimi kwa upande wangu naona kufungia redio za dini ni kuficha tatizo kwa sababu zifuatazo

1. Mpaka sasa hatujaambiwa kwa kuongea maneno haya au kwa uchochezi wa dini kwa maneno haya ndio yaliyopelekea kufungia redio hizo

2.Kama ni kweli kuna maneno watakayotuambia kwamba ndio yamepelekea redio hizo zifungiwe waliyoyasema maneno hayo wamechukuliwa hatua gani au vyombo vya redio vilisema vyenyewe?

3.Kufungiwa kwa gazeti la Mwana Halisi hatujaambiwa kwa kuandika habari hii ndiyo iliyopelekea gazeti kufungiwa na hata kama kuna hizo habari zitakuwa zimejiandika zenyewe mpaka gazeti lifungiwe?yule alieandika habari hizo amechukuliwa hatua gani?

4.Kuna kiongozi mmoja wa CCM amesema anawafahamu watu wanaopanga mauaji tena maneno hayo anayasema hadharani lakini polisi awambani ili aeleze anaachwa tu,

5.Kuna viongozi wa CCM wanasema wazi mbele ya watu kwamba chadema ni chama cha wachaga polisi wanashindwa kuwapana watoe ushahidi maana hairuhusiwi chama cha kikabila

6.Viongozi wa CHADEMA wanasema CCM ni chama cha mafisadi na walifikia mpaka kuwataja lakini polisi wanashindwa kuwabana watoe ushahidi maana hairuhusiwi kuwa na chama cha kifisadi

7.Pengo amesema ameambiwa na watu anaowaamini kuhusu kulipuliwa bomu Arusha lakini polisi wanashindwa kumbana aeleze ukweli
yote haya utakuta wanakamatwa watu wengine kuhusiana na matatizo niliyoainisha hapo ndio maana nasema yanayofanyika ni kuficha matatizo badala ya kuyamaliza nawakilisha
 
Mimi Bubu Msemaovyo siongei lakini Naandika!!!
 
ndo hivyo serikali dhaifu inajifunika blanketi la udini ili ipendwe
 
​WaTz ni watu wa ajabu sana. Hivi kuficha ficha ukweli wakati inafahamika ni dini gani wanao fanya fujo kunawasaidia nini? You guys got to grow up and man up.

Eti nitakuwa nakuja JF kuangalia post za udini. My foot.
 
Back
Top Bottom