Kufungua kampuni ya udalali

flulanga

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2016
Posts
4,860
Reaction score
6,390
Habari ndugu zangu.

Baada ya kusikia habari kutoka serikalini kuwa na madalali wanatakiwa kuwa na leseni ya biashara ya udalali ndio utakuwa unafanya shughuli zako kihalali.

Nimeona fursa hapo kutokana na madalali sio wote ila wengi sana wanaendesha biashara zao bila ya kufuata taratibu za serikali inavyotaka, mimi nimeona nifanye hii biashara kihalali kabisa kwa kufuata taratibu zote.

Nataka nifanye kihalali sio kwasababu yakuiogopa serikali ila nataka niaminike kwawateja wangu nawajue napatikana wapi.

Vilevile nataka nifate taratibu zote ili niwe huru kupambania dili kubwa kubwa zaserikali au makampuni na mabenki endapo wanapoamua kuuza mali zao au za watu kwa njia ya mnada basi na mimi niwe na vigezo vya kugombania tenda hizo.

Nataka nifanye kisasa kabisa niwe na ofisi kabisa. Niwe na camera na kompyuta kwa ajili ya kuhifadhia kwa picha mali zinazouzwa ikibidi na video kabisa kwa ajili mteja anapokuja ofisini unamuonesha kama ni nyumba kuuzwa basi mteja unamuonesha mazingira yote ya hilo eneo lenye nyumba na majirani kabisa wa hilo eneo na viwanja nihivyo hivyo na vitu vingine ili hata mnapoamua kwenda site au kwenda kumuonesha kile unachokiuza basi unakuwa na asilimia zaidi 75% ya kumuuzia mteja uliyenaye kwa wakati huo.

Najua wapo madalali ambao walisha development ila naamini kabisa bado niwachache sana.

Nachohitaji mnishauri. Nifungue kama kampuni na nikatie leseni ya biashara yakampuni navipi gharama zake? Au nifungue kwa jina la kawaida yaani kwa majina yangu na leseni nikate ya kawaida? Kipi kizurii na chenye unafuu kati ya hivyo viwili?

Msaada wenu wazoefu wa mambo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sababu kuu uliyotumia kuingia kwenye soko la udalali/Biashara husika haiko sustainable unaweza fanya hivyo ila ni suala la muda madalali wote wakongwe watajisajiri na wao kuwa rasmi kama wewe.
 
Naomba nielezee
1. Masuala ya usajili, gharama na uendeshaji wake
2. Changamoto zake
3. Uzoefu wangu

1. Usajili, Gharama na Uendeshaji wake

A: Utangulizi
Biashara ya udalali ie Commission agent ni biashara kama biashara yoyote ile inayoingiza kipato halali na ni ya heshima tu. Dalali ananufauka na kiasi cha pesa au asilimia fulani sio lazima bhasi kila biashara inayopita mkononi mwako iwe ni lazima upate 10%. Kuna mambo mengi ya kibiashara ya kuangalia ili mteja umchaji kiasi fulaninikiwa pamoja na hali halisi ya kiuchumi. Changamoto kubwa imekuwa kwa wanaoifanya wengi kutokuwa waadilifu au kutaka hela kubwa sana kutokana na tamaa au kutokuwa na weledi nk. Hali hii imefanya biashara ya udalali kuwa ya kitapeli na watu wasioaminika katika jamii

A: Kusajili kampuni vs Jina la biashara
Unaweza kusajili kampuni au kusajili jina la biashara - BRELA. Faida za kusajili kampuni ya udalali ni kuwa inakuongezea thamani ktk kazi zako hasa unapoomba tenda katika makampuni mengine. Gharama za usajili kwa kampn inategemea na mtaji uliotaja ktk Memart

Ukishapata cheti cha usajili cha kampuni au vyeti vya jina la biashara utaenda TRA. Kama kampuni ina maana utapewa TIN ya kampuni baada ya kuwasilisha vielelezo vyote vinavyohitajika na kama jina la biashara TIN kama unayo tyr itaongezwa jina ulilosajili la biashara na kulipia kodi uliyojikadiria (kampuni) au kukadiriwa (binafsi). Utaomba Tax Clearance kwenda BRELA kwa ajili ya leseni ya udalali ie Commission Agent ambayo ni laki 3 na kuomba online ie TNBP

Then utaanza kuoperate biashara yako
Ili kufikia malengo yako vema na kujitofautisha na madalali wengine ni vema ukafanya haya:
1. Kuwa na ofisi nzuri inayoeleweka na kuwa siriasi kuepuka ofisi yako kuwa kijiwe cha madalali
2. Andika wasifu wa kampuni ie company profile
3. Andika barua za maombi ya kazi za udalali kutokana na unachofanya huku ukiambatanisha na wasifu wa kampuni
4. Acha mazoea ktk biashara hii
5. Kuwa na mashine ya EFD kwa ajili ya kutoa risito kwa malipo stahiki unayolipwa

2. Changamoto za biashara ya udalali
1. Utoaji wa risiti
Hili kuwa makini maana ukishaaminiwa na wateja malipo ya jumla yanakuwa yanapita kwako hvy hakikisha unatoa risiti ya kile kiasi tu unachonufaika nacho ww na mhusoka mkuu anatakiwa atoe kiasi chake husika. Mfano: kuna kazi ya mil 2 lkn hela yako ni laki 1 basi toa risiti ya laki 1. Kukosea kutoa hapo ina maana mauzo yk yatakuwa juu hivyo kupelekea kuja kulipa kodi ya mapato kubwa. Lkn pia kuna kodi ya huduma ya 5% usiisahau

2. Uaminifu
Madalali wengi ktk jamii wamekuwa na wanaonekana si waaminifu. Unatakiwa ujue kuwa ktk biashara hii jamii inakuangalia kwa sura ya kutokuwa mwaminifu. Basi jitahidi uweke mazingira ya uaminifu

3. Kuletewa wateja na madalali wenzako
Sio jambo baya ila hakilisha umejiridhisha na mteja hy na mqelezw kuwa hy aliemleta kwako hahusiki kwa lolote na kampuni yk kwn kutofanya hayo ipo siku atatapeliwa huko na msala kurudi kwako. Chukua tahadhali hii

Nk hizi ni za haraka haraka

3. Uzoefu ktk biashara ya udalali
Hii biashara nimeifanya sana hsa upande wa malori ya mizigo upande wa TRANSIT CARGO. Inalipa sana lkn lazima uwekeze sana hasa technolojia ndiyo utaweza kuimudu vema kuanzia
1. Kupata mikataba ya malori ambayo wao wanakuwa wanaleta docs ofisini kwako masua yote ya kutafuta mizigo i abaki kwako
2. Kuwa na mikataba na makampn ya clearing and forwading kukupa mikataa ya uhakika ya mizigo
3. Ulipaji usio wa kusumbua japo hali si hali
4. Kwa na connections za mizigo ya kurudi toka nje ya Tz
5. Kuhakikisha unafanya daily tracking ya malori yote uliyopakia mizigo na kuwasilisha ripot asbuhi na jioni kwa walengwa nk
6. Kuwa na mtaji wako ambapo iwapo kuna chnagamoto imetomea bhasi unaimaliza then unakuja kudai ktk utaratibu stahiki wa kihasibu nk nk

Kwa kuyafanya haya nilijitofautisha kabisa na madalali wa mizigo woote na kufanya biashara vema kabisa
Kwa haya machache kuna yenye manufaa kwako yafanyie kazi


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante mkuu kwakushare uzoefu wako, Naomba unikaribishe pm siku nikihitaji msaada wako zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Karibu sana Mkuu
Pia zipo kampuni za udalali tumezisajili na zinafanya kazi vema katika sekta za
1. Usafiri majini
2. Usafiri nchi kavu
3. Masuala ya ardhi
4. General business

Sent using Jamii Forums mobile app

Naomba nitumie Watsapp namba yako nikuulize maswali kidogo tukielewana nakua mteja wako


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Vizuri umekuja kiongozi

Naitaji kujua je auction brokers anaweza jihusisha na udalali wa kuuuza na kununua au kuna utofauti?
Hawa ni madalali wa ukusanyaji wa madeni, kusimamia uuzaji wa mali za wale walioshindwa ktk mikopo ktk kuuza mali zao kwa mwongozo wa sheria. Hawahusiki kununua mali ya mteja na kisha kuiuza
 
Kwaiyo boss nikiitaji kudeal na udalali wa nyumba, thamani na viwanja pamoja na huo wakukusanya made naitaji kampuni kuisajili vipi?
Hawa ni madalali wa ukusanyaji wa madeni, kusimamia uuzaji wa mali za wale walioshindwa ktk mikopo ktk kuuza mali zao kwa mwongozo wa sheria. Hawahusiki kununua mali ya mteja na kisha kuiuza
 
Kwaiyo boss nikiitaji kudeal na udalali wa nyumba, thamani na viwanja pamoja na huo wakukusanya made naitaji kampuni kuisajili vipi?
Hy ni commission agent. Kudeal na masuala hayo wewe unakuwa mtu wa kati kuunganisha deal mbalimbali kisha inachukua 10% yk kazi ikikamilika. Ina maana utakuwa na leseni hii

Pia kama na auction broker itabidi uwe na uelewa wa sheria kama faida kwako kwa kuwa mambo mengi yanatokea mahakamani
 
Shukrani mkuu takutafuta mtaani kuna pesa ipo inazagaa zagaa naona kwa jicho hili naweza Fanya jambo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…