Kufungua tawi la chadema udom

Tumekupata vilivyo Miradibubu,umetutia ahueni kidogo.
Tutatoa hata michango ya mali kufanikisha hilo.Ikumbukwe kwamba Dodoma ni ngome kuu ya CCM,hivyo inahitajika nguvu za ziada.Nawapongeza CHDEMA UDOM,kwa jitihada zinazoendelea hapo.Ni wazo zuri ofisi ziwe mjini kati pale,coz naamini mtapata wageni wengi sana toka sehemu mbalimbali za nchi hapo tawini.Ningependa tu kuwaomba muwe chachu kwa matawi mengine hapo dom,ni dhahiri matawi mengine,pamoja na CDM Mkoa,bado ni dhaifu sana hapo dom,Tumeshuhudia hayo wakati wa kampeni.Msifanye kazi kama tawi tu la UDOM,Tunaomba mfanye kazi kama ya operation pia,Enendeni mpaka jimbo la Bahi,kule upinzani haupo kabisa na Badwel mbunge wa ccm alipita kiulaini kabisa,ni mbunge mzuri na zahitajika nguvu za ziada kuvunja ngome yake,ni wasomi kama nyinyi mnaweza kulikomboa.Nasema mwende kila jimbo la dom coz nyie mchanganyiko wa watu mbalimbali toka kona mbalimbali za nchi,so haitatosha mkifanya kazi kama tawi tu,mkaikomboe Mvumi pia.Lakini nina wasiwasi mahala fulani,wingi wenu wanachadema hapo UDOM,Ungetosha kabisa kuchukua jimbo la mjini 2015,endapo wakati wa kupiga kura mngekuwa DOM,kama kawaida CCM watakifunga chuo wakati wa kupiga kura ili msipige kura,hapo ndipo tutalikosa jimba tena,sijui mmejipangaje.Pale SAUT Mwanza temefanikiwa kuifukuza CCM kabisa mkoa wa Mwanza na ni kwa jitihada za wanaCDM tawi la SAUT.Sasa tunafanya jitihada kuifukuza CCM kanda nzima ya ziwa na hilo tutalithibitisha uchaguzi ujao.Tuko nyuma yenu kwa hali na mali.
 
Haya ni mapambazuko yenye kutia matumaini, moyo huo wa kimapinduzi mkiuelekeza kwa vijana wanaosoma kwenye shule za yeboyebo pindi mpatapo nafasi, CCM haita himili NGUVU YA UMMA 2015. Ni aibu kwa kijana wa kisasa kukumbatia CCM inayofilisi nchi hii..


Mapambano yote yataendelea kama kawaida na moto tunaoenda kuuwasha hauwezi kuzimwa na mwanadamu yeyote
 

Nimeipenda sana mistari hiyo iliyo kwenye red. Umesahau kusema ukiona baadhi ya members wachache hapa ni CCM ujue ni vichwa wazi. Teh teh teh teh teh.Ninakupa big up!
 
Hongereni vijana. Nchi hii itajengwa na vijana wenye moyo wa dhati. Never Give up!
 
Nilichukia sana chuo hiki kwa sababu wachakachuaji walituaminisha ni chao na waliomo chuoni ni wao.
Miradibubu umenifariji sana. Naweza kusema tu tupo pamoja. Chadema oyeeeeeeeeeeeeeeeeeee hakuna kulala mpaka kieleweke.
 
mawenzi,

chelea chelea utakuta mwana si wako.

mimi ni mwalimu mipango dodoma na nina kadi ya chadema, na wala sijifichi kwani naamini katika demokrasia na maendeleo baada ya kugundua kuwa hakuna dalili yoyote ya mapinduzi.

pia tuko wengi, ni uhuru wa raia. bora tu usivunje sheria ya utumishi.

sijifichi, na naringia hilo. karibu tujiunge. ukiona vipi nenda pale majengo sokoni, karibu na cana lodge annex ndio ofisi ya mkoa. chukua kadi yako na anza kuringa mara moja!
 
Miradibubu mimi binafsi nimekuamini 100% kutokana na ukweli uliouweka hapa. Kwanza umesema Gilead Terry kada wa ccm alieshindwa urais Udom,huyu kijana namjua vizuri tangu anasoma Loyola high school pale mabibo dsm ni mccm damudamu. Pia yule Thobias Mwesiga uliemsema bila kumtamka wazi namjua pia,yeye kasoma Rubya seminari kwa miezi 7 kisha akatimuliwa kwa uhuni. Umesema kweli,sisi wanachadema tutawapa nguvu kadri ya uwezo wetu. Hata kama hatuna fedha kama mafisadi ccm,tutatumia elimu zetu kuikomboa Tanzania. Viva Miradibubu,aluta continua!
 
Höngera sana wana udom kuingia upinzani.
Ila wajameni huyu mtoa mada ananitia shaka na jina lake la miradi bubu! Je, huu mradi wake wa tawi ni wa kweli au bubu?
Bw/Bi. Miradi bubu nakuomba uanzishe mradi wa ukweli ambao utakuwa chachu ya kuamsha vijana wa kitanzania hasa wasomi. Ninaomba agenda kubwa iwe umoja na uzalendo wa kweli ambao utalenga kuboresha maisha ya kila mtanzania.
Ningependa pia ktk tawi hilo paibuke watu kama Dr. Slaa ambao wataanza kuibua uozo ktk utawala wa Udom maana nasikia kuna miungu watu huko ambao wanafanya mambo yasiwe shwari.
Pia ningependa suala la udini lilohuburiwa sana na baadhi ya viongozi kpnd cha kampeni kama mtaji wao wa kukusanya kura lishughulikiwe ktk ngazi ya tawi ili kuvunja uzandiki na unafk wa mafisadi.

Hongereni sana. Cha msingi tuweke uzalendo na utu mbele, na chachu ya maendeleo iwe kwa maslahi ya umma na sio mtu binafsi. La sivyo kuna hatari ya kugeuka toka wepesi hadi wazito!!

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Udom!
 
Ondoa shaka juu ya hili jina kwani limetokana na riwaya moja tamu sana inayoibua ufisadi wa CCM tangu Azimio la Arusha mpaka kusambaratika kwake, Riwaya hiyo inaitwa Miradi Bubu ya Wazalendo ambayo imeandikwa na Prof. Gabriel Ruhumbika, Ukiweza jaribu kuisoma inatueleza wapi tulipo iacha njia
 

Tupo pamoja mkuu ninyi ndio wadau wenyewe na pasipo watu kama wewe hatutafika mbali, mapambano yanaendelea
 
jana nilikuwa katika afisi za CHADEMA za mkoa na nimepata taarifa zote.

ni kweli vijana wa udom wamenzisha tawi pale makulu - kata ya chadema. PIA NASIKIA WAMEMTIMUA yulE MWENYEKITI WAO aliyeenda kuchuana na nimrod halafu akapewa pesa akajitoa.

nimesikia hata kina salva rweyemamu na kina ridhiwani wanawapiga mkwala viongozi wa wanafunzi kuwa wako chadema.

tawi liko hai.
 

umetumia vigezo ambavyo kisomi havikubaliki, wot im sayin is, wazo mlilo nalo ni zuri, but next tym unapotaka kupresent idea yako, iweke kisomi zaid, huwezi sema mabishano ya kwenye mabasi ni fact ya kukuonesha nyie ni wanaharakati, mlikua wapi kipindi kile moja ya kikundi cha wanafunzi wa Udom walivyokua wanaikashifu Chadema na dr. slaa, au hata kuponda kile kitendo cha kutoka bungeni,, anyway this no time for lawama, i gues my point umeinasa, wishin you luck in bringing devpt to dis rich poor country.........................
 
Safiiiiiii!! Hii nimeipenda sana, binafsi nilikuwa siamini propaganda za ccm kuwa udom wana wanchama wengi.Ni wazi, hakuna mwenye akili timamu akawa mwanachama wa ccm unless otherwise awe kibaraka wa mafisadi, na hao vibaraka ndio hatuwataki kabisa hao ni hatari zaid ya ukoma hao.uarabuni hao adhabu yao ni kitanzi tu!

HONGERENI SANA VIJANA, MKIPANGA TAREHE RAISMI MTUJURISHE TUJE KUWAPA SUPPORT!! BIH UP KUBWA!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…