Kufunguliwa kwa awamu ya nne ya udahili

Kufunguliwa kwa awamu ya nne ya udahili

Ralphsams

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2020
Posts
347
Reaction score
350
Baada ya kukamilika kwa awamu zote tatu za udahili, Tume imepokea maombi ya kuongeza muda wa udahili kutoka kwa baadhi ya waombaji waliokosa udahili kutokana na sababu mbalimbali.

Pia, Tume imepokea maombi ya kuongeza muda wa udahili kutoka kwa baadhi ya Taasisi za Elimu ya Juu nchini ambazo bado zina nafasi katika baadhi ya programu za masomo kwa mwaka 2021/2022.

Ili kutoa fursa kwa waombaji ambao hawakuweza kudahiliwa au hawakuweza kuomba udahili katika awamu tatu zilizopita kutokana na sababu mbalimbali, Tume imeongeza muda wa udahili kwa kufungua Awamu ya Nne na ya mwisho ya udahili inayoanza leo tarehe 11 Oktoba hadi 15 Oktoba, 2021.

Tume inawaasa waombaji wote ambao bado hawajadahiliwa, watumie fursa hii vizuri ili kupata nafasi ya udahili.
 
Back
Top Bottom