Kwa wanaowajua vizuri matapeli na wachumia tumbo wachuuzao na kuuza roho yaliyokata tamaa, kufunguliwa kwa duka la Gwajima ni ushahidi tosha kuwa lao ni moja.
Hivyo, sitashangaa serikali ikipiga fedha yetu kulipa fidia ili wagawane nasi tupigwe. Iweje 'makosa' yasamehewe bila adhabu wala kuwajibika kama hakuna namna?
Mwenzenu nahuzunika, kushangaa, na kuhoji kimya kimya. Kweli, ukishangaa ya Musa, utaona ya Firauni!