Kufungwa inauma sana, tuchukue hii kama fundisho

hapakazit

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2015
Posts
839
Reaction score
663
Habari wana jamvi to decrare interest mimi ni mshabiki wa simba lilia na matokeo ya jana yameniuma sana na kama mnavyojua Kufungwa inauma sana.

Ila kwa upande mwingne bora tumefungwa huyu mtu anaitwa haji manara ajifunze anaiona simba kama tim ya malaika kutoka mbinguni fc isiyofungwa anatukana na kudharirisha watu anatisha na kutukana waandishi hasa wanawake kitendo alichofanya wiki iliyopita sio cha ki ungwana bahati mbaya hakuna aliejitokeza kumuonya anajivunia ulemavu wake manara amekuwa mjinga siku hiz bora tumefungwa ajifunze tumepoteza mchezo inauma sana ila acha tujifunze kuwa na akiba ya maneno na nidham tunapoongea na watu wengne na hiii ni laana itatufuna.

Na natamani huu ujumbe umfikie Manara anadharirisha club yetu ya wastaarabu kwa sababu ya ulemavu wake watu wanamuogopa kumsema kwa kuwa yeye ni mlemavu wa ngozi.

Huwezi kumdharirisha mwanamke ukabaki salama. Acha lizame na ubingwa tukose iwe fundisho kwake ngoma ikuvuma sana mwisho hupasuka acha ipasuke.
 
Ki ukweli huyo Haji manala serikali/wadau wa mpira wa miguu wana muogopa, na ni kutokana na ulemavu wake huo, na ndio hutumia hicho kichaka kudharirisha watu wengine!!!il siku ile msemaji wa Yanga alipomtolea uvivu watu wakaja juu sana!!ila ipo siku tu ataleta maafa.

Tatizo lake ameshawafahamu mashabiki wa simba wanata kusikia nini, na yeye anapitia humo humo, kuwajaza upepo!!kitu kinachopelekea kuingia uwanjani na matokea yao!!Na ikitokea simba wakampiga chini ataishi maisha ya tabu kutokana na jinsi anavyowachukulia waandishi wenzake.
 
mi ni mshabiki wa yanga ila kitendo cha afisa habari wa timu kulumbana na waandishi wa habari ni kitu cha ajabu sana hasa kwa timu zinazojinasibu kuwa zinataka kujiendesha kibiashara, hakuna wachambuzi wanaokera na kuudhi km kwe media za ulaya ila huwez timu ikawa busy kubishana nao, wawekezaji km MO wako pale kibiashara so issue ya public relation ni muhimu sana
 
Pole mkuu ndo mpira. Mtaani sasa baridiiiiii!!!!!![emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Hatuna Shabiki mshamba kama wewe.Kaa kimya,matokeo na Haji wapi na wapi??
Soma vizuri uzi wangu Mungu ana njia nyingi za kulipa kilio cha watu hivi uliona manara alivyomjibu Prisca kishamba kwa. Wapenzi na wadau wa mpira wa miguu kile kitendo sio cha ku ki entertain na duniani hakuna tim. Isiyofungwa manara anatujaza nimeumia sana kufungwa na utopolo ila kumdharirisha mwandishi tena aliepo kazin uliemualika mwenyewe imeniuma zaidi
 
Kwanza kwa kauli zile sikutegemea atakuwa ofisin hadi leo
 
Anachofanya manara ndicho kinachohitajika, mpira unahitaji amsha amsha na ndio maana derby ya kariakoo ni moja kati ya derby tano kubwa Africa .. ila manara ameenda extra mile, anahitaji kuwekwa chini na kufundishwa maadili ya kazi yake ..

Sent from my itel W5002 using JamiiForums mobile app
 
Hawajui ilo wenyewe Leo akijitoa wanaenda kumbembeleza!!

Brand yeyote alichokifanya Manara alitakiwa kufutwa kazi
 
Kama kuna shabiki wa Simba ahamini kwamba Simba itafungwa basi ahamie timu isiyofungwa,kuhusisha kufungwa kwa Simba na Haji ni mbingu na ardhi avihusiani kabisa.
 
Hebu washabiki wa simba tukubali kuwa yanga walituzidi mbinu wakashinda tuwape heshima maana hakuna timu isofungwa mbona prisoni na ruvu walitufunga.

Tusilaumu mtu hapa hata wachezaji walijitahidi kucheza ila tulizidiwa mbona.

Tusemapo kuwa Simba ni Team kubwa mojawapo ni kuwa na mashabiki tunaokubali simba yaweza pia kufungwa na mpira una matokeo 3

tuwaheshimu Yanga walituzidi mbinu tukafungwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…