Magufuli 05
JF-Expert Member
- May 7, 2023
- 1,433
- 2,791
Sina kumbukumbu sahihi kuwa ni lini wafanyabiashara wa Kariakoo wamewahi kugoma kwasasabu yoyote. Kariakoo ndiyo Dubai ya nchi yetu, ina wafanyabiashara wa kila aina, wakiwemo wenye mitaji mikubwa, ya kati na midogo.
Kikubwa zaidi wanajitambua, naamini hawawezi tu wakakurupuka kugoma bila kuvumilia na kufika mwisho. Hapa ni kwamba tatizo hili limeanza zamani, wamejitahidi kwa namna moja ama nyingine kuihusisha serikali lakini imeshindikana.
Lakini kilicho nisikitisha zaidi ni madai yao kwamba Bandarini kuna urasimu. Daaa, aibu iliyoje, kama ni kweli kuna urasimu kwenye lango kuu la uchumi na biashara za nchi yetu, tunakwenda wapi? Nchi nyingine zinatamani kuwa na bandari kama yetu tu, ili ziweze kulisha Afrika yote, sisi kuna urasimu?
Tunakwenda wapi, mbona hatukuyaona haya awamu ya tano? Rais JPM aliweka macho yote pale,mambo yalikuwa shwari, mbona ghafla hivi? Changamoto wanazopitia wafanyabiashara wa kariakoo ndiyo hizo wanapitia wafanyabiashara nchi nzima.
Serikali hii ni sikivu kweli?
Serikali hii ina nia ya dhati kweli?
Serikali hii mbona mambo yapo vululu valala kiasi hiki?
Nchi hii tunaipeleka wapi?
Mungu isaidie na Watanzania amkeni. Wakati ni sasa wakujenga nchi yetu kwa kuondoa wasioweza kuongoza na kuchagua wale wenye dhamira ya kweli.
Mungu ibariki Tanzania.