kichenchele
JF-Expert Member
- Jun 28, 2010
- 539
- 176
Japo lengo huenda lisiwe kama tunavyodhania lakini hizi timu zinazotumia huo uwanja zinatia aibu,uwanja haujaanza kufungwa leo,na wangekuwa ni watu wa kufikiri sasa wangeshakuwa na viwanja siku nyingi kwa mfano Simba na Yanga wanaweza kuweka tofauti zao pembeni wakashirikiana kutafuta wabia wengine wakakodi uwanja (e.g Tanganyika parkers) hata kwa miaka 10 wakaukarabati ili wautumie kwa mechi za ligi tu,hatua kwa hatua wanaweza kujikwamua na kuondokana na adha hii. Hata Ulaya kuna timu hazina viwanja ila zimeingia mikataba ya kuvimiliki na kuvitumia ktk mechi zao.Ni ishara kuwa kila timu iwe na uwanja wake mzuri unaofaa kwa mechi za ndani na za kimataifa. Sio kukalia majungu na ufisadi tu!