Kufurahi na marafiki 'club'

Kufurahi na marafiki 'club'

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841

Club ni eneo la starehe linalokusanya watu mbalimbali kupata vinywaji na kuburudika na mziki, usiku kucha.

Watu mbalimbali; waajiriwa, wafanyabiashara n.k baada ya kupambana mchana kutwa, katika kujipatia kipato; hutumia muda wa jioni au usiku kwenda kuburudika na vinywaji au kucheza mziki maeneo ya 'club'

Sifa ya 'club' nzuri ya kutembelea​
  • Iwe na mazingira mazuri na yakuvutia​
  • Iwe na uwazi wa kupata hewa safi​
  • Iwe na walinzi, mabaunsa n.k​
  • Iwe na wahudumu safi na amabao wako shapu​
  • Vinywaji vyao viwe bei juu kiasi, ili daraja la watu wastaarabu ndio waweze kuingia.​
Anayefaa kwenda 'club'​
  • Yeyote mwenye kipato cha kulipa bill
  • Aliyestaarabika​
  • Mtu aliye smart kichwani, mwilini na mavazi​
Utakaowakuta 'club'​
  • Waajiriwa​
  • Wafanya biashara​
  • Wazee wa mjini n.k​
Muda upi wote walioko club wanakuwa na mawazo yanayofanana?​
  • Kuanzia saa 8 usiku na kuendelea, wote walioko 'club' waliokunywa pombe, nyama choma n.k huwa wanaongea lugha moja.​
  • Kama una vibes, unaweza kutengeneza network kubwa sana, kwasababu utapata nafasi ya kuzungumza na yeyote mle ndani; awe ana cheo, ameajiriwa, amejiajiri n.k​
Watoto wakali 'pisi kali'​
  • Wote walioingia 'club' wanaamini yeyote aliyemo ndani na anakunywa vinywaji; atakuwa na pesa ya kulipa bill,ingawa pia wapo wenye salio la kunywa chupa mbili tu​
  • Watoto wakali wapo wa kutosha, waliojiajiri, ajiriwa n.k​
  • Muhimu mfuko wako uwe umetuna kiasi, ukiwa na laki mbili au zaidi sio mbaya.​
Namna ya kumtongoza 'pisi kali' anayejilipia mwenyewe bill
  • Wapo warembo wakali, ambao hawapendi kutumia hela ya mwanaume; wakiamini wao wako vizuri kiuchumi.​
  • Kama utamuona mtu wa namna hiyo,na akauteka moyo wako, we mfuate, kisha muambie hivi:-​
  • ' Inakuwaje mtoto mzuri hivi, unakunywa pombe peke yako na wakati sisi tupo?' akionyesha tabasamu, muulize anatumia kinywaji gani? Kisha muagizie halafu ondoka kwenye hiyo meza ukakae peke yako na kuendelea na vinywaji vyako. Mlipie vinywaji mpaka yeye aseme basii; kisha mfuate mpeane namba za simu; yatakayojiri mtajuana wenyewe.​
  • Pia kujiimarishia usalama, ni vizuri pia hata wale mabaunsa ukawalipia vinywaji; watakupa heshima kubwa zaidi ya kufurahi na marafiki.​
Kwa hayo tu; nendeni mkafurahi na kulewa na marafiki, sio kila muda kuwaza kununua matofali tu.​
 
Kuleni maisha vijana kabla hamjaondoka hapa duniani. Maisha yenyewe ndiyo haya haya.
 
Back
Top Bottom