Kufutwa kwa pori tengefu la Msomera, watetezi wa mazingira mko wapi?

Kufutwa kwa pori tengefu la Msomera, watetezi wa mazingira mko wapi?

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2022
Posts
3,891
Reaction score
8,448
Pori tengefu la Msomera mkoani Tanga limefutwa rasmi na Serikali na sasa litapangiwa matumizi mengine ikiwemo kuwapa wamasai wanaohamishiwa kutoka Mbugani ambako wamefurushwa ili kumpisha mwarabu ajenge mahoteli.

Kinachoshangaza zaidi ni watu waliojitanabaisha kuwa ni watetezi wa mazingira kukaa kimya bila kupinga kwa pori hili ambalo limekuwa chanzo cha maji kwa muda mrefu.

Wakati ulipotangazwa ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Mwl. Nyerere mara moja watetezi wa mazingira kutoka ndani na nje ya nchi waliibuka na kupinga ujenzi huo kwa sababu utasababisha uharibifu mkubwa wa mazingira.

Je, kufuta pori tengefu la Msomera siyo uharibu wa mazingira ila ujenzi wa bwawa ni uharibifu wa mazingira?
 
Nalifuatilia kwa ukaribu sana hili na majibu nitaleta nimekaa pale👉 loading..............
 
Hao watetezi siyo wajinga, hata wao utamu was asali wanaujua.
 
Back
Top Bottom