Kufuzu AFCON 2017: Chad vs Tanzania

Deogratius n

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2015
Posts
1,193
Reaction score
254
CHAD VS TAIFA STARS
Date:23.3.2016
Time:15hours EAT

Timu ya Taifa Stars leo itakuwa uwanjani kupambana na timu ya Taifa ya Chad kwenye kombe la mataifa Afrika

Nahodha mpya wa Taifa Stars ya Tanzania Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu ni tegemeo kubwa kwenye mechi na Chad.

Taifa Stars ni ya tatu kundi G na pointi moja tu kwa mechi mbili walizocheza, ya kwanza walifungwa mabao matatu bila kisha wakaenda sare na Super Eagles ya Nigeria.

Misri inaongoza kundi hilo na pointi sita, Nigeria ya pili ikiwa na pointi nne.

KIKOSI CHA TAIFA STARS NA CHAD LEO NI:-
1. Aishi Manula
2. Kapombe
3. Haji Mwinyi
4. Erasto Nyoni
5. Kelvin Yondani
6. Himidi Mao Mkami
7. Thomas Ulimwengu
8. Jonas Mkude
9. Mwinyi Kazimoto
10. Mbwana Samatta na
11. Faridi

Akiba
1. Mostapha
2. Mohamed Tshabalala
3. John Boko
4. Ajibu,
5. Kichuya,
 
STARS KAMILI KUWAVAA CHAD KESHO

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager kimekamilika baada ya kundi la pili lenye wachezaji nane kuwasili leo mchana nchini Chad tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya wenyeji kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2017.

Kundi hilo la pili limewasili majira ya saa sita mchana (saa za Chad) likiongozwa na mkuu wa msafara ambaye pia ni Rais za ZFA, Ravia Idarus na kupokelewa na viongozi waliopo jijini N’Djamena.

Mara baada ya kuwasili D’jamena wachezaji walipata nafasi ya kupumzika hotelini kabla ya kuelekea mazoezini kufanya mazoezi ya pamoja kwa wachezaji wote, yakiwa ni mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo wa kesho.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars Charles Mkwasa amekiongoza kikosi chake chenye jumla ya wachezaji 20 kufanya mazoezi mepesi saa 9 mchana katika uwanja wa Idriss Mahamat Ouya uliopo jijini N’Djamena.

Katika mazoezi ya leo wachezaji wa Taifa Stars walionekana kuwa na umakini mkubwa katika kusikiliza maelekezo ya kocha Mkwasa, huku morali ya wachezaji ikiwa juu kuelekea kusaka pointi 3 muhimu katika mchezo huo.

Wachezaji waliopo Chad ni magolikipa Aishi Manula na Ally Mustafa, walinzi Shomari Kapombe, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Mohamed Hussein, David Mwantika, Erasto Nyoni na Kelvin Yondani.

Viungo ni Himid Mao, Jonas Mkude, Mwinyi Kazmito, Mohamed Ibrahim, Farid Musa, Deus Kaseke na Shiza Kichuya, huku washambuliaji wakiwa ni John Bocco, Ibrahim Ajibu, Thomas Ulimwengu na nahodha Mbwana Samatta.

Mechi kati ya Chad dhidi ya Tanzania inatarajiwa kuchezwa kesho Jumatano saa 9:30 (saa 11:30 kwa saa za Tanzania) katika uwanja wa Idriss Mahamat Ouya jijini N’Djamena, na utarushwa moja moja na kituo cha luninga cha Taifa cha Chad (Tele Chad).

Chanzo: Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
 
Hii match inaoneshwa na kituo chochote cha tv hapa nchini?
 
Anayefahamu hii game inaoneshwa Chanel gani?
 
hii mech siielew ipo au haipo mpk sa iv kimya,super sport channel karibu zote nehi
 
lakini ile ya Algeria walionyesha nje ndani via TBC2 ila leo hapa sioni dalili aisee
hyo TBC2 si wanaona wachache mkuu, chukua mfano wa wenzetu Kenya game zao zote lazima uzione KBC hamna cha KBC one wala KBC two
 
Kwa saa za bongo mechi itaonyweshwa saa 12 jioni kupitia dstv
 
...acheni moto subirini muda ufike ndio muanze kulia lia,kwanza sijui ni lini mara ya mwisho hao TBC walionesha mpira,welcome Rioba.!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…