Kufuzu Fainali za CHAN: Tanzania 1 - 1 Rwanda

craq

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2017
Posts
859
Reaction score
1,866
TAIFA STARS VS RWANDA

Leo nyasi za dimba la CCM Kirumba, Jijini Mwanza, zitawaka moto pale Timu ya Tanzania 'Taifa Stars' itakapowakaribisha Amavubi Timu ya Taifa ya Rwanda katika mechi ya kuwania kufuzu fainali za mashindano ya Mataifa Africa kwa Wachezaji wanaocheza ligi za ndani CHAN.

Utabiri wako unahusika nani ataibuka Kidedea?

Kikosi cha TAIFA STARS kinachoanza dhidi ya RWANDA 'Amavubi'' (CHAN)

Saa 10: 00 Jioni / Live ZBC 2

1. Aishi Manula
2. Shomari Kapombe
3. Gadiel Michael
4. Nurdin Chona
5. Salumu Mbonde
6. Erasto Nyoni
7. Saimoni Msuva
8. Himidi Mao
9. John Bocco
10. Mzamiru Yassin
11. Shiza Kichuya

Akiba

Said Nduda
Boniface Maganga
Tamimu Abdulkarim
Salmin Hoza
Raphael Daudi
Stamil Mbonde

========

Haya ni Matokeo kati ya Taifa Stars vs Rwanda kuwania Kufuzu Michuano ya CHAN Leo 15.7.2017

HALF TIME
Taifa Stars 1 - 1 Rwanda (19' Nshuti,33' Himid Mao bao la penati ) .

FULL TIME
Taifa Stars 1 - 1 Rwanda (19' Nshuti,33' Himid Mao bao la penati )

Matokeo ni Tanzania 1 - 1 Rwanda
 
Manula chunga sana Said Mohamed, la sivyo utavuna mabua.
 
Kuna siku niliwaza sana baadaye nikajikuta naomba msamaha kwa Mungu.

"Kwa vile soka letu linaonekana kuwa kichwa cha mwendawazimu, nikawaza siku moja ndege itakayowabeba wachezaji ipotee kama ya Malaysia ili tuanze upya huwenda haya maigizo ya kuamini kuwa wachezaji wa timu ya taifa lazima wawe ni wale wa simba yanga,Azam".

Sasa Bokko anasimamishwa kweli hadi sasa kama mshambuliaji wa kutegemewa! Kweli !!!!!!.

Haaaa Na lazima tufungwe.

Sent From Samsung S9 edge using JamiiForum mobile app
 
Hamna kocha mle.
Kwa mataji yapi kupewa National Team
Bora angekuwa Mecky Maxime angalau. Ndiyo kocha mzawa aliye achieve the highest position kwenye VPL
 
Pitch ya kirumba ina mapungufu sana...mpira hautulii

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Halftime 1-1

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Update please....

Sent from my SM-G903F using JamiiForums mobile app
 
kama upo kichwani kwangu....wachezaji hata kucontrol mpira hawawezi yaan wanarukaruka tu uwanjani bora serengeti boys mpira wao ulikuwa unaonekana
 
Ka Kichuya kanarukaruka tu kama kitenesi

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…