Bado tunaweza kuwa na Sherehe za Siku ya Uhuru kwa bajeti yoyote ile iliyopangwa na mambo mengine yakaendelea kama yalivyopangwa.
Ni dharau kwa Watanzania wazalendo kama akina Cognizant (alias), Adorable, Angel kufuta sherehe za uhuru na kusema pesa zielekezwe katika matumizi ya jambo lingine.
Najua kila mwaka kuna pesa za maafa ambazo huwa ziko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na hurudishwa Hazina na zingine huishiwa kutafunwa kwa kutengenezewa maafa ya kiusanii tu.
Hivi kama kweli tunaipenda Tanzania yetu ni kwanini sherehe za uhuru zisiwe zinaendelea kwa bajeti iliyopangwa na kama kuna pesa inayohitajika kwingineko basi hii chenji ya hela ya maafa inayotengwa kila mwaka (ninayoambiwa ni nyingi mno) isitumike huko? Lakini utamaduni wetu wa kizalendo wa kusheherekea uhuru wetu wa 9 Desemba kwa shamrashamra mbalimbali usiendelee?
Walioipigania hii nchi hawakuwa mazuzu kupenda kusheherekea hii siku muhimu kwa Tanzania na Watanzania pamoja na kwamba wa kipindi chao uchumi wa nchi ulikuwa ni mbaya hata kuliko sasa.
Kwenda kinyume nao ni kujitakia tu laana za makusudi halafu baadaye taifa likiwa na nuksi nyingi na mabalaa mengi, wale wale waliozuia kufanyika kwa sherehe za uhuru wanahaha kwa Watanzania na viongozi wa dini mbalimbali (tena wakiwa na nyuso zao za huruma) wakiomba taifa liombewe.
Tuache kuidharau siku ya uhuru wetu.