Kugombea na kutumia gharama kubwa ukijua hutoshinda, ni sawa na kutogombea?

Kugombea na kutumia gharama kubwa ukijua hutoshinda, ni sawa na kutogombea?

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam!

Je, ni sawa kupanga kujenga mnara pasipo kukaa chini na kupiga hesabu juu ya gharama zake?

Siasa ni sayansi, je ni sawa chama Cha siasa kumpitisha mgombea asiyekubalika ,asiyekidhi matakwa ya wapiga kura?

Ni sawa kuleta mgombea asiyependwa na wananchi?

Ni sawa kupeleka n'gombe aliyekonda mnadani tukitegemea kupata Bei nzuri sokoni?

Je, kupeleka mgombea au kupeleka jeshi vitani Ukiwa huna silaha na uhakika wa kushinda vita ni uamuzi sahihi?

Nauliza vyama vya siasa, wananchi wakifanikiwa kudai reforms kwenye Katiba na kupata Tume huru ya Uchaguzi, tutaendelea na mgombea aliyepo au tutambadili?

Kugombea na kutumia gharama kubwa ukijua hutoshinda, ni sawa na KUTOGOMBEA?

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Nawasilisha!
 
Uchaguzi ni vita kama vita zingine,

Si vyema kufanya majaribio kwenye uchaguzi,

Kupeleka mgombea dhaifu, ni kuweka chama kwenye hatari ya kufutika.
 
Ni kupoteza muda na rasilimali, huyo Samia hata JPM akifufuka leo maadam ni mgombea wa CCM basi atamshinda JPM kwa 90% na hapo ndio watu wataamini kwanini chadema inasema no reform no election.

Hata hao kina Polepole na Mpina wacha wajitoe CCM wakipata 10% ya kura za ubunge ndio wataamini kuwa uchaguzi sio huru. Natamani kampeni hii iwashawishi zaidi wana CCM wenye ndoto za kugombea ubunge na urais nje ya CCM kama wagombea binafsi au upinzani kwamba watakua na uhakika wa kushinda hata wakijitoa.

Cha ajabu wanadhani reforms zitainufaisha chadema bila kujua siku wakifanyiwa figisu CCM na kufukuzwa ndio wataona umuhimu wa tume kuwa huru.
 
Uchaguzi ni vita kama vita zingine,

Si vyema kufanya majaribio kwenye uchaguzi,

Kupeleka mgombea dhaifu, ni kuweka chama kwenye hatari ya kufutika.
Mgombea dhaifu ndio yupi? Hata Trump wote walijua hawezi toboa ila alishinda. Kwahiyo acha wadhaifu na wenye nguvu wagombee, na wananchi wataamua kidemokrasia, msiwapangie.
 
Mgombea dhaifu ndio yupi? Hata Trump wote walijua hawezi toboa ila alishinda. Kwahiyo acha wadhaifu na wenye nguvu wagombee, na wananchi wataamua kidemokrasia, msiwapangie.
Kumbe ni sawa kupanga kujenga mnara bila kupiga hesabu juu ya gharama zake?

Na ikipatikana Tume huru ya Uchaguzi,vyama vitarudi kubadili wagombea Ili kuendana na ushindani?
 
Yaani mkt mstaafu CDM, angejua atashindwa vita, Bado angechukua fomu kugombea?

Sasa kugombea ukashindwa, Kuna tofauti na KUTOGOMBEA?
 
Back
Top Bottom