Ni wanandoa kwa miaka 15 sasa, kwa miaka 4 mume alikuwa na nyumba ndogo (jirani yake) bila mke kujua. Mke alipogundua alifungasha virago kutaka kurudi kwao ila mume alimzuia na kumuomba msamaha. Mke hakukubali msamaha kirahisi hivyo mume aliwashirikisha baadhi ya marafiki zake wa karibu kumshawishi mkewe kukubali msamaha wake. Mke akamsamehe yakaisha. Baada ya msamaha mume amebadilika hatoi matumizi kwa familia kuanzia chakula, matibabu na ada. Haki ya ndoa kwa mke imekuwa msamiati. Mke amedata anaona ndoa chungu na amekata tamaa.
Waungwana naomba tumshauri wenzetu. (Ni ndg yangu wa karibu).
....kwenye masharti ya msamaha ndipo kwenye walakini, muulize tena 'aliweka' masharti gani kiasi kwamba huyo baba kabadilika? (huenda kaambiwa watoto si wake je?)
Mambo ya ndoa ni magumu sana ( very complex and complicated). Mwenye kosa akiwa mwanaume, mwanamke unatakiwa utumie busara sana kwanza kupima na kujua unataka nini:
1.Kama bado unamtaka mumeo, ukiombwa msamaha na ukakubali uhakikishe ni baina yenu tu na haihusishi mtu wa tatu.( bakiza siri kati yake na wewe) Hapo uhusiano una chance kubwa ya kubaki mzuri au hata bora kuliko ilivyokuwa.
2. Kama na wewe ushamchoka na hujali matokeo, basi unaweza kumkoromoea utakavyo na hata ukashirikisha watu wengine kujadili tatizo lenu na kupata ufumbuzi.Ila ukae tayari kukubali sasa kunyanyaswa zaidi maana haogopi kitu tena.Kama ni siri alikuwa anatunza, haipo tena na wewe sasa unajua kwa hiyo hajali chochote tena.
Hapa aliyeshika mpini ni mume na makali kayashika mwanamke.Mmoja wao akivuta atakayeumia ni mwanamke.
3. Wanaume wana kisasi na kinyongo sana.Wanawake wanasamehe kirahisi.Hivyo huyo mwanamke aamue tu kama anataka kuendelea kuishi maisha hayo ya kero.Kama alikuwa anamtegemea huyo mume kwa kila kitu basi imekula kwake.
Hima,WoS, wazo la kushirikisha marafiki kwenye kutatua tatizo lilikuwa la mume hivyo kama alikuwa hapendi watu wajue asingeshirikisha marafiki zake!
Mke anafanya kazi ndio maana ameweza ku-handle mahitaji ya familia for that long, but amechoshwa, maisha ni magumu kwa yeye kubeba jukumu la kutunza familia all alone.
Hima,
Huyu bwana alikuwa anatafuta gia ya kumfanya aelewe ukweli na kafanikiwa.Inaelekea huyo bwana ni wale wabinafsi sana...anajua kuwa huyo mke anaweza kutunza familia - watoto wote wanne na ndiyo maana akafanya jitihada za kuhakikisha haondoki.Maadam mke anajimudu na alikuwa tayari kumrudia mumewe basi mpira uko kwake kimaamuzi.Ingekuwa mimi ningejiondosha nikaanza maisha mapya bila huyo mume.

WoS, hauko mbali sana na ukweli kwenye hili swala la ubinafsi coz mme yuko radhi kusadia ndg kuliko kusomesha wanae!
Mke kujimudu kunafikia kikomo maana gharama za maisha hasa ada ya watoto ni kubwa na anahofia wanae wanaweza kukosa shule na baba yao hajali hilo!
Kama anafanya kazi huyo mwanamke na ana kipato kinachoweza kulea watoto na yy mwenyewe, mie naona bora atengane na huyo jamaa. Hizi ndoa jamani, hadi wengine tunaogopa kuingia ktk ndoa.
Mshauri ausikilize moyo wake unavyomtuma halafu aamue.Anavyozidi kuzubaa kwa huyo bwna ndivyo anazidi ku deplete resources zake ambazo angeweza kuzitumia kusomesha wanae.Na je yuko na uhusiano mzuri na hao watoto wa kufikia?
Uhusiano na watoto na kufikia ni mzuri coz mke aliwalea tangu wakiwa wadogo na sasa wako sekondari.
Hima,
Huyu bwana alikuwa anatafuta gia ya kumfanya aelewe ukweli na kafanikiwa.Inaelekea huyo bwana ni wale wabinafsi sana...anajua kuwa huyo mke anaweza kutunza familia - watoto wote wanne na ndiyo maana akafanya jitihada za kuhakikisha haondoki.Maadam mke anajimudu na alikuwa tayari kumrudia mumewe basi mpira uko kwake kimaamuzi.Ingekuwa mimi ningejiondosha nikaanza maisha mapya bila huyo mume.
Jamani wanaume ni wakatili sana na sijui hii tabia yao itakoma lini,kama mke alimsamehe na kuamua kubaki kwa nini amfanyie hayo?Au lengo lake ilikua ni mkewe apate taarifa kuwa ana mtu mwingine ili amnyanyase vizuri? Nahisi pia huyu mama anampenda sana jamaa na ndo maana jamaa anafanya hayo kwa makusudi kwa kuhisi kuwa hata akifanya kosa ataomba msamaha na atasamehewa na maisha yataendelea,maana what i know ni kwamba mwanaume akishajua kuwa mke anampenda sana inakuwa tabu.
wanaume wengine ovyo sana, sasa unatembea na jirani maana yake ni nini? adabu hakuna hata kidogo jamani, loo