Kugunduliwa kwa chanjo ya UKIMWI nchini

Kugunduliwa kwa chanjo ya UKIMWI nchini

Kafyulilo

Senior Member
Joined
Feb 8, 2013
Posts
106
Reaction score
70
Gazeti la Mwananchi la leo limeripoti kugunduliwa kwa chanjo ya UKIMWI nchini likielezea tafiti zilizofanywa na hospitali ya Mhimbili tangu mwaka 2007 hadi 2012, zikihusisha askari polisi na magereza wapatao 60 ambao walipewa hiyo chanjo na wakaachwa kuishi maisha ya kawaida kwa muda wa miaka mitano. Inaelezwa kwamba utafiti huu pia uliwahusisha wananchi wa kawaida wapatao 60 kati ya mwaka 2008 hadi 2012, kutoka jijini Mbeya. Na imegundulika kwamba hawakupata madhara yoyote wala hawakupata maambukizo ya virusi

Hoja ya msingi katika utafiti huu ni kwamba wahusika walipewa kinga, halafu wakaachwa kuishi maisha ya kawaida, na baadaye kuwapima tena kuona kama wamepata maambukizi. Kutokana na haya wanafanya hitimisho kwamba chanjo ya UKIMWI imegundulika. Binafsi naona huu ni ulaghai: Ama gazeti la Mwananchi halijaripoti taarifa yote kama ilivyoripotiwa na Professor Bakari ambaye aliongoza utafiti huu, au matokeo ya utafiti huu ni ya kimagumashi. Na nitashangaa kama jumuia ya Ulaya imeridhishwa na matokeo ya utafiti huu bila kuhoji.

Ninazo sababu kadhaa za kupinga utafiti huu!

  1. Sample size iliyotumika kwa clinical research hairidhishi kwa kuwa likelihood ya watu 60 kuishi na kujiachia kwa miaka mitano bila kupata maambukizi ni kubwa sana. Kwa Pandemic disease kama AIDS, hatukupaswa kufanya hitimisho kwa sample ya watu 60 tu au hata kama wangekuwa 1000 pengine wasingetosha hasa ukizingatia kwamba ni asilimia tano tu ya watanzania wana maambukizi.
  2. Ikumbukwe kuwa kwa kila tendo la ndoa tunalofanya na mtu mwenye maambukizi, likelihood ya kupata maambukizo ni asilimia 2 tu. Na kwa mtu ambaye ametahiriwa, likelihood inaweza kupungua zaidi. Kwa hiyo kama hawa askari 60 waliopewa chanjo walifanya ngono na wanawake au wanaume wenye maambukizi lakini kwa matayarisho mazuri na ya kutosha, ni wazi likelihood ya asilimia mbili iliwapita pembeni
  3. Ninaamini kwamba pamoja na kupewa chanjo, hawa askari walikuwa pia wana tahadhari ya mimba, na matokeo mengine ya ngono, nje ya UkIMWI, je ni kwa kiasi gani watafiti wamejiridhisha kwamba hawa askari hawakutumia kinga nyakati zote? Na je ni kwa kiasi gani wamejihakikishia kwamba hawa askari walitembea hata na wanawake au wanaume wanaojulikana kuwa ni waathirika?
  4. Matokeo ya utafiti hayatuambiii kama hawa askari sitini walihojiwa na kuonyesha kwamba walijiachia hovyo na wanawake au wanaume walioathirika, tena bila kutumia kinga?
  5. Utafiti haujatuambia walikuwa ni watu wa maadili gani, maana yawezekana waliopewa hii chanjo walikuwa ni wale waliooa na wanaoheshimu ndoa zao, wacha Mungu au kama walikuwa hawajaoa basi walikuwa na wachumba zao na wanaishi kwa uaminifu na wachumba zao. Ni kwa vipi tunaweza kufanya hitimisho kwamba chanjo imegunduliwa?
Binafsi napata kigugumizi kutokana na aina hii ya uandishi wa habari ambao unaweza kuwafanya watu wakabweteka wakiamini kwamba chanjo imegunduliwa kumbe ngoma bado mbichi. Kwa mitizamo wangu kilichogunduliwa si chanjo, bali ni usalama wa hiyo dwa ya chanjo. Badala ya kusema chanjo imegunduliwa, wangeweza kusema dawa ya chanjo imethibitika kuwa haina madhara kwa binadamu, then utafiti unaohusu uthabiti wa hiyo dawa katika kukinga dhidi ya UKIMWI ungeweza kuendelea.
 
Sina utaalamu sana wa clinical researches, lakini huku kwenye social science researches, sample ya 60 kwa experimental research huwa ni ok. Sema labda control ya mazingira ndiyo haipo clear kwenye utafiti wao. Wanajihakikishiaje kwamba hawa askari walifanya ngono na wenye virusi?
 
Back
Top Bottom