MwanaHaki
R I P
- Oct 17, 2006
- 2,401
- 707
Waungwana
Habari za asubuhi? Natumai wote hamjambo.
Kuna kampuni ninataka kufanya nayo biashara. Wanaonekana kuwa "genuine" lakini nimefanya utafiti juu yao kwenye Google jana. Kampuni inaitwa Quingdao Unique Products Development Co. Limited, iliyoko kwenye jimbo la Quingdao, China.
Kampuni hii imejitangaza ipasavyo kiasi kwamba ukifanya Google Search, utapata references nyingi zinazoisifia kuliko zinazoiponda. Hata hivyo kuna references mbili za kuonya kwamba kampuni hii ni ya KITAPELI.
Ninachotaka kujua ni:
Nasema yote haya kwa kuwa miaka kadhaa ya nyuma niliwahi kuagiza (Euro 250) kifaa kimojawapo kwa ajili ya mashine ya imagesetting (mliopo kwenye printing industry mtanielewa. Pesa zilienda, kifaa hakikutumwa, nikaonekana tapeli. Lakini niliwaeleza wahusika walioniagiza na kunipa pesa zao ili niagize kifaa hicho, na kuwaonesha ushahidi wa taarifa ya Benki (SWIFT), ili wajue kwamba sikula pesa zao.
Kufanya biashara na kampuni za China haswa kwa njia ya elektroniki, yataka moyo na ujasiri. Nyingi ni za kitapeli. Watafanya kila jitihada kuhakikisha unatuma pesa; wataonekana very genuine, kumbe wapi.
Wadau mlio na uzoefu zaidi nisaidieni kwa hili. Nimekwama.
Asanteni.
P.S. Mwenye jibu la uhakika tafadhali tuwasiliane kwa njia ya PM.

- Uhalali wa kampuni hii, kwa kuihakiki nikiwa hapa nchini, yaani, kupitia Ubalozi au wakala wa kibiashara wa China. Je, ninafanyaje? Nimetumiwa email kadha wa kadha kwa biashara ninayotaka kuifanya, na INALIPA.
- Nataka kuhakiki details za Benki wanayoitumia. Ninafanyaje? Inawezekana kwamba wana akaunti kwenye hiyo Benki, na pesa zikatumwa, lakini wengi wa hawa watu huwa wanadai kwamba watumiwe pesa kwa jina la mtu, si la kampuni, na haswa kupitia Western Union. Kama wamtumia pesa mtu usiyemfahamu kupitia Western Union, ni sawa na kutupa pesa chooni. Kama ni tapeli, hutaipata hiyo pesa.