Kuhakiki Uhalali wa Kampuni za Kichina zinazotangaza kufanya biashara mbali mbali

MwanaHaki

R I P
Joined
Oct 17, 2006
Posts
2,401
Reaction score
707
Waungwana

Habari za asubuhi? Natumai wote hamjambo.

Kuna kampuni ninataka kufanya nayo biashara. Wanaonekana kuwa "genuine" lakini nimefanya utafiti juu yao kwenye Google jana. Kampuni inaitwa Quingdao Unique Products Development Co. Limited, iliyoko kwenye jimbo la Quingdao, China.

Kampuni hii imejitangaza ipasavyo kiasi kwamba ukifanya Google Search, utapata references nyingi zinazoisifia kuliko zinazoiponda. Hata hivyo kuna references mbili za kuonya kwamba kampuni hii ni ya KITAPELI.

Ninachotaka kujua ni:

  1. Uhalali wa kampuni hii, kwa kuihakiki nikiwa hapa nchini, yaani, kupitia Ubalozi au wakala wa kibiashara wa China. Je, ninafanyaje? Nimetumiwa email kadha wa kadha kwa biashara ninayotaka kuifanya, na INALIPA.
  2. Nataka kuhakiki details za Benki wanayoitumia. Ninafanyaje? Inawezekana kwamba wana akaunti kwenye hiyo Benki, na pesa zikatumwa, lakini wengi wa hawa watu huwa wanadai kwamba watumiwe pesa kwa jina la mtu, si la kampuni, na haswa kupitia Western Union. Kama wamtumia pesa mtu usiyemfahamu kupitia Western Union, ni sawa na kutupa pesa chooni. Kama ni tapeli, hutaipata hiyo pesa.

Nasema yote haya kwa kuwa miaka kadhaa ya nyuma niliwahi kuagiza (Euro 250) kifaa kimojawapo kwa ajili ya mashine ya imagesetting (mliopo kwenye printing industry mtanielewa. Pesa zilienda, kifaa hakikutumwa, nikaonekana tapeli. Lakini niliwaeleza wahusika walioniagiza na kunipa pesa zao ili niagize kifaa hicho, na kuwaonesha ushahidi wa taarifa ya Benki (SWIFT), ili wajue kwamba sikula pesa zao.

Kufanya biashara na kampuni za China haswa kwa njia ya elektroniki, yataka moyo na ujasiri. Nyingi ni za kitapeli. Watafanya kila jitihada kuhakikisha unatuma pesa; wataonekana very genuine, kumbe wapi.

Wadau mlio na uzoefu zaidi nisaidieni kwa hili. Nimekwama.

Asanteni.

P.S. Mwenye jibu la uhakika tafadhali tuwasiliane kwa njia ya PM.
 
Mkuu mbona ni essy, wewe fikia nao maamuzi na waambie utalipia kupitia Escrow, kama ni matapeli hapo ndo utakapo wakamatia, Escrow ni systeam ya alypay ambapo ukisha ikia makubaliano na muuzaji una gerester online na pesa utatuma kwao na wo watoa pea kwa muuzaji pale tu muuzaji atakapo releae mzigo,

Jaribu kuwaambia utalipia kupitia alpay, wakigoma ndo hapo, kuna njia nyingine za kuwatambua
 
mimi mwenyewe nilishatepeliwa japo sio kampuni uliyoitaja ila kuwa muangalifu sana, nina imani mwenye kujua zaidi atajitokeza
 
Kwenye online business watu waaminifu ni wajapan tu. Hawa wengine magumashi njenje.

Kama biashara hiyo ni muhimu na ni reasonable volume, funga safari uwatembelee otherwise ni kamali tu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…