Kuhamia Dodoma na fursa za kibiashara

maroon7

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
11,311
Reaction score
15,640
Wakuu,
Kufuatia hatua ya serikali kuhamia Dodoma ni wazi kwa sasa huo ndio mji unaoweza kuwa na fursa nyingi za kibiashara kuliko mji wowote hapa Tz. Sababu ipo wazi watumishi wengi wanazidi kuhamia kwa kasi na bado hapo mabalozi na HQ za taasisi nyingine kama mabenki,tfda,tbs etc hazijaenda.
Binafsi nampango wa kwenda ku-survey mwezi july ili kuangalia fursa zipi za kibiashara zinaweza kuwa nzuri na ikiwezekana nihamie kabisa ili kwenda sambamba na ukuaji wa haraka wa mji wetu mkuu.
Naomba tuungane hapa hasa kwa waliopo Dom kutoa changamoto na fursa mbalimbali zilizopo kwa sasa kuanzia kodi za frame,nyumba,upatikanaji wake na hata sehemu muhimu ambazo mtu anaweza akatega kitu kama mini-supermarket,hardware,pharmacy,salon,
boutique,car wash,garage,duka la vipodozi,butchery, n.k.
 
Upo mkoa gani?
 
Hope so, isije kuwa km mtwara maana wanasiasa hawakawii kuchenji gia hewani , ukaskia wameamua kubaki dar kwa muda ikawa ntolee
aha ha a umeniwahi, ukiwa mjasiriamali bongo usiendeshe mambo kwa kauli za politicians, unajiachia mazimaa unakuta washakwepa hilo anguko lake sio la dunia hii,just imagine
1.mji mpya wa kigamboni
2. Ntwara gas
3. machinga complex
na blabla zingine.
Hata hili la dodoma mtu lazima uingie kwa Umakini sana.
 
kumbuka kuhamia dodoma ni kwa shughuli za kiutawala na watumishi wa dodoma tu, kama reli itajengwa dodoma hasa kwa shughujliza ujenzi itakuwa na inakuwa
 
Unatafuta partner kutoka nje ya nchi? au unataka kuuza huduma/bidhaa zako ndani na nje ya nchi?
Basi, kutana na viongozi wa biashara wanaonadi biashara zao kupitia mtandao wa lenkeer.com.
Jiunge Bure sasa hii na upate nafasi ya kushida account VIP bure yenye thamani ya $200!
JIUNGE SASA NA USHINDE. https://www.lenkeer.com/register
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…