Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama nakumbuka; mnaingia mkataba wa mauziano kwa mwanasheria then mwende Polisi ukajiridhishe bunduki hiyo haina soo lolote, umpate mtaalamu aikague ufanyaji kazi wake (firing order) hili muhimu sana, halafu mtaiacha huko (Armoury) kwa matunzo baada ya wote kuridhiana (omba ilainishwe na kusafishwa kabla ya kuiacha). Mtarudi kusaini makubaliano kwa mwanasheria yeye atachukua chake na wewe utarudi Polisi kuacha nakala yako ya mauziano na kuanza utaratibu wa kupata leseni ya umiliki na kununua risasi mpaka utapopata basi utajitwalia mwanzi wako kwa matumizi sahihi kwa mujibu wa sheria za nchi...
ONYO; BUNDUKI SIO FIMBO UMILIKI WAKE UNAHITAJI UMAKINI NA MABADILIKO YA TABIA NA MIENENDO YAKO KWA UJUMLA. JIANDAE KWA HAYO KABLA HUJAAMUA
KUMILIKI BUNDUKI.