KERO Kuhamishwa kwa machinjio Morogoro - kero ya wachinjaji

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wachinjaji wa Manispaa ya Morogoro tunaambiwa mpaka tarehe 17.08.2026

Tunatakiwa kuhamisha shughuli zetu za uchinjai kwenye machinjio mpya iliyojengwa na Manispaa eneo la mawasiliano kata ya mkundi licha ya machinjio hyo mpya iliyojengwa na manispaa kutokukidhi vigezo.

Manispaa walilazimisha ujenzi huo kwenye eneo lililokuwa limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa machinjio ya kisasa ambayo ilitakiwa kujengwa na Wizara ya Kilimo na ufugaji kutokana na taarifa yao waliyowahi kuichapisha kwenye website yao.

Manispaa wamejenga machinjio isiyokidhi vigezo licha ya sisi wafanyabiashara wa nyama kulalamika ubora wa machinjio hyo pamoja na ubovu wa barabara ya kutoka main road hadi kufika kwenye machinjio hiyo

Tumeilalamikia manspaa ubovu wa miundo mbinu hiyo hasa nyakati za mvua lakin hakuna kilichorekebishwa mpaka sasa.

Je, kama wameshindwa kurekebisha miundo mbinu na kuboresha mazingira ya machinjio hiyo kabla hatujahamishwa hivi wataweza wakati ambao washatuhamisha.

Tunaomba mtuwasilishie kero yetu hatujui hatma yetu ni ipi mpaka kufikia hiyo tarehe.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…